Habari za Punde

WAZIRI MWAKYEMBE AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA NORWAY

Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akimsikiliza mmoja wa wataalam walioambatana na Balozi wa Norway nchini Tanzania Mhe. Hanne Marie Kaarstad (wa tatun kulia) walipomtembelea ofisini kwake leo
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria Prof. sifuni Mchome (wa pili kulia) akifafanua jambo wakati wa kikao na Balozi wa Norway na ujumbe wake (hawapo pichani) walipotembelea Wizara hiyo leo ili kujadili namna wataalam hao wanavyoweza kusaidia kiteknolojia katika kurahisisha upatikanaji wa haki kwa wananchi.
Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiagana na Balozi wa Norway nchini Tanzania Mhe. Hanne Marie Kaarstad na ujumbe wake baada ya kumaliza kikao leo jijini Dar es salaam. 
Picha na Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.