Habari za Punde

WENYE SALUNI ZENU MTASUBIRI SANA KIPINDI HIKI,MHE RIDHIWANI YEYE ANAMSUKA MTOTO WAKE MWENYEEEEWE

Mbunge wa Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete akiweka kando shughuli nzito za kujenga Taifa na kubeba majukumu ya mzazi kwa kuketi chini na kumfumua nywele binti yake Aziza Tamika Kikwete kabla ya kusukwa upya nyumbani kwake Chalinze. 
Mhe Ridhiwani ameiambia Globu ya Jamii kwamba kwake yeye hilo ni jambo la kawaida kabisa kwani anasema anatambua umuhimu kwa viongozi kupata muda na kukaa na familia nyumbani kwani kuna maisha baada ya uongozi. Aziza mwenye unri wa miaka 7 na ambaye ni mtoto wa kwanza wa Mhe. Ridhwani, kachukua jina la bibi yake yaani mama wa baba yake.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.