Habari za Punde

YANGA YAIRARUA ASHANTI UNITED MABAO 4-1 KOMBE LA SHIRIKISHO

Winga wa Yanga Simon Msuva, akimiliki mpira mbele ya beki wa beki wa Ashanti Unted Patrick James,wakati wa mchezo wa Kombe la Shirikisho uliopigwa jioni ya leokwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Katikamchezo huoYanga waliibuka na ushindi wa mabao 4-1. Picha Zote na Muhidin Sufiani wa Mafoto Blog
 Mshambuliaji wa Yanga Amis Tambwe,akichuana kuwania mpira na beki wa Ashantu United wakati wa mchezo wa Kombe la Shirikisho.
 Kiungo wa Yanga Deus Kaseke akiwania mpira na beki wa Ashanti United, Seleman Sultan.
*****************************************************
Mabingwa watetezi wa kombe la  Azam Sport, Yanga wameanza  kampeni yake ya kutetea taji hilo baada ya kuifunga timu ya daraja la kwanza ya  Ashanti United  mabao 4-1.
Kutokana na ushindi huo, Yanga sasa imeingia hatua ya 16 bora ya mashindano hayo ambayo mwaka huu yameshirikisha jumla ya timu 80 za madaraja tofauti.
Katika mchezo huo uliofanyika kwenye uwanja wa Uhuru, Ashanti ilianza kwa kasi, lakini kwa kadri muda uliyokuwa unakwenda, wachezaji wake walionekana kushindwa kuhimiri mikikimikiki ya wachezaji wazoefu wa Yanga.
Dakika 10 za mwanzo, Ashanti ilicheza vizuri, lakini ilipoteana baada ya kufungwa bao la kwanza katika dakika ya 17 lililowekwa kimiani na Amissi Tambwe kufuatia pasi safi ya Simon Msuva.

Bao hilo liliwachanganya sana wachezaji wa Ashanti na kuifanya Yanga kutawala mchezo. Makosa ya kipa wa Ashanti, Rajabu Kaumbu liliiwezesha Yanga kupata bao la pili katika dakika ya 36 kupitia kwa Thabani Kamusoko kwa shuti la mita 35 baada ya ‘kumchungulia kipa huyo aliyekuwa amesogea mbele.
Baada ya bao hilo, Ashanti walijitutumua sana, lakini wachezaji wake walikosa umakini kutumia nafasi kadhaa za wazi walizozipata.

Ashanti ilianza kipindi cha pili kwa kasi na kufanya mashambulizi kadhaa, lakini ikajikuta ikipachikwa bao la tatu katika dakika ya 52 kwa njia ya penati baada ya beki wa kushoto wa timu hiyo, Seleman Sultan kumkwatua Msuva ambaye alikuwa anakaribia kufunga.

Msuva alifunga bao la tatu. Ashanti ilijitahidi na kupata bao la kwanza katika dakika ya 61 kupitia kwa  Isack Hassan kufutia makosa ya beki wa kati wa timu hiyo, Vincent Andrew.

Bao hilo liliwashtua Yanga na kufunga bao la nne katika dakika ya 89 kupitia ya Yussuf Mhilu kufuatia makosa ya kipa wa Ashanti United aliyeshindwa kuzuia vizuri mpira wa krosi wa Emmanuel Martin.

Katika mchezo huo, bechi la ufundi la Yanga lilifanya mabadiliko ya kikosi ambapo kwa mara ya kwanza, Oscar Joshua alicheza nafasi ya beki wa kati.
 Juma Mahadhi akiruka kupiga mpira wa kichwa huku beki wa Ashanti United, Patrick James,akijaribu kumdhibiti. KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
 Simon Msuva akipiga mpira wa kichwa huku Patrick James akimkwepa
 Kiungo wa Ashanti United, Abeid Kisiga, akijaribu kuwatoka mabeki wa Yanga, Oscar Joshua na Said Makapu.
 Kipa wa Ashanti Hussein Mkongo kiondia moja ya hatari langoni kwake.
 Deus Kaseke akimpongeza Thaban Kamusoko baada ya kutupia bao zuri la shuti kali alilopiga umbali wa mita zaidi ya 35.
 Amis Tambwe akituliza mpira kifuani
 Simon Msuva akipongezana na Juma Mahadhi
 Amis Tambwe akishangilia bao lake
 Juma Mahadhi akichuana na Patrick James
 Mahadhi na mabeki wa Ashanti
 Mahadhi na mabeki wa Ashanti
 Thaban Kamusoko akitoa pasi ya kisigino
 Kaseke akichuana na Seleman Sultan
 Kaseke akichuana na Seleman Sultan 

Yusuf Mhilu,akishangilia bao lake
 Kikosi cha Ashanti United:  Rajabu Kaumbu, Hussein Kondo, Seleman Sultan, Patrick James, Peter Mutambuzi, Zam Kuffor, Abeid Kisiga, Sharif Mohammed, Isack Hassan, Yahaya Zaydi, Rajab Mohamed
 Kikosi cha Yanga: Beno Kakolanya, Juma Abdul, Haji Mwinyi, Oscar Joshua, Andrew Vincent, Saidi Juma, Simon Msuva/Yussuf Mhilu, Thabani Kamusoko, Juma Mahadhi/Mathe Anthony, Amissi Tambwe/Emmanue Martin`, Deus Kaseke.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.