Habari za Punde

WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI WAWEKAWAZI KUHUSU MFUKO WA KUWAWEZESHA WATUMISHI WA UMMA KUMILIKI NYUMBA

 Mkurugenzi wa Idara ya Nyumba Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Michael Mwalukasa akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu mfuko wa kuwawezesha watumishi wa Serikali kumiliki Nyumba ambapo zaidi ya watumishi 2000 wameshanufaika na mikopo yenye riba nafuu ya asilimia 3 ili kuwawezesha kumiliki nyumba bora. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Mikopo ya Nyumba Bi Lucy Kabyemera na Kushoto ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo Bi Fatma Salum.
Mkurugenzi Msaidizi Mikopo ya Nyumba,Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bi Lucy Kabyemera akifafanua kwa waandishi wa habari kuhusu faida wanazopata watumishi wa Umma kutokana na mikopo inayotolewa na Serikali ili kuwawezesha kumiliki makazi bora.  Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Nyumba Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Michael Mwalukasa. Picha na Frank Mvungi-Maelezo

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.