Habari za Punde

ZIARA YA KIKAZI YA NAIBU WAZIRI MASAUNI WILAYANI NKASI KUTEMBELEA IDARA ZA WIZARA

 Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana na maafisa wa Jeshi la Polisi baada ya kuwasili wilayani Nkasi kwa ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kupitia shughuli zinazofanywa na idara zilizopo ndani ya wizara yake na kubaini changamoto wanazokutana nazo na kuzitafutia ufumbuzi.Kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Said Mtanda. 
Afisa Uhamiaji Wilaya ya Nkasi, Juma Khamis Ali (kushoto), akikabidhi taarifa ya Idara yake kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, wakati wa ziara ya kikazi ya Naibu Waziri huyo wilayani humo ikiwa na lengo la kupitia shughuli zinazofanywa na idara hizo  na kubaini changamoto wanazokutana nazo na kuzitafutia ufumbuzi.Wengine pichani ni wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wilayani humo.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wafanyakazi wa idara zilizopo ndani ya wizara yake(hawapo pichani), wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya wilayani Nkasi ikiwa na lengo la kupitia shughuli zinazofanywa na idara hizo  na kubaini changamoto wanazokutana nazo na kuzitafutia ufumbuzi. Wengine pichani ni wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wilayani humo
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Said Mtanda(kulia) akizungumza na  wafanyakazi wa idara zilizopo ndani ya wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi (hawapo pichani),wakati akimkaribisha Naibu Waziri wa Wizara hiyo ,Mhandisi Hamad Masauni(wapili kulia) wakati wa ziara ya kikazi aliyoifanya Naibu Waziri huyo wilayani humo.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(wakwanza kulia), akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza kikao cha ndani na watumishi wa idara zilizopo chini ya wizara yake wilayani Nkasi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.