Habari za Punde

AMA KWELI WAKAZI WA KIGOGO NI MANUNDA AISEE HILI TANGAZO ETI HAWALIONI AISEE

  Pamoja na Halmashauri kuweka tangazo hili katika eneo hili la Kigogo CCM pembezoni mwa barabara Kigogo kuelekea Manzese au Mabibi, lakini bado Wakazi wa maeneo haya wamezidi kuwa ni wenye ukaidi uliopitiliza ambapo huendelea kumwaga na kurundika Taka eneo hili tena mbele ya bango lenye Tangazo linalowakataza kumwaga Taka eneo hili tena lenye mkwara mzito wa kumpiga faini kila atakayeonekana akitupa taka.
Lakini pia pamoja na wahusika kuweka Tangazo hili je, ndiyo basi mmemaliza? ina maana Tangazo hili linatosha kulinda na kumkamata atakayemwaga Taka? Haya sasa kama bango hili hutosha kwa ujumbe na kumzuia raia kumwaga taka basi badilisheni aina ya ulinzi kama huu kwani tayari aina hii ya bango imeshindwa kuwakamatia wanaokiuka kwani linawaona wakimwaga lakini halina uwezo wa kuwakamata..... ni mawazo tuuuuu
Wameshawadharau na bangolenu sasa....

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.