Habari za Punde

ASKOFU GWAJIMA AACHIWA JIONI YA LEO ATOKA KITUONI AKICHEKELEA

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima (katikati) akiongozana na baadhi ya wasaidizi wake wakati akitoka kituo cha Polisi Kati baada ya kuachiwa ambapo alikaa ndani huku akihojiwa kwa siku mbili kuanzia juzi mchanaa mpaka leo mchana.

Gwajima ni miongoni mwa watu 65 waliotajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda, akiwataka kuripoti Kituo cha Polisi Kaati kwa ajili ya maahojiano kuhusu kuhusika kwa namna moja ama nyingine na biashara ya Madawa ya kulevya.

Aidha Askofu huyo aliripoti kituoni haapo siku ya Alhamisi mchana akiwahi siku moja kabla na ile iliyotangazwa na mkuu wa Mkoa ambayo ilikua rasmi ni siku ya jana Ijumaa,lakini pamoja na kuripoti kabla Gwajima alianza kuhojiwa siku hiyo hadi anaachiwa jioni ya leo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.