Habari za Punde

ASKOFU GWAJIMA AZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KABLA YA KUTUA POLISI LEO

 AKIZUNGUMZA na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo. wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josepahat Gwajima amekana kuhusika na biashara ya madawa ya kulevya na kusema kuwa ameokoka na anamtumikia mungu hivyo kutajwa katika orodha ya wanaojihusisha na dawa za kulevya iliyotangazwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ni jambo ovu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Askofu Gwajima amesema kuwa Mkoa wa Dar es Salaam anafanya kazi vizuri lakini suala la kiutawala hawezi na kumuomba Rais Dk. John Pombe Magufuli ambadilishie kazi.
Amesema yeye alikuwa Mpwapwa katika kazi zake aliposikia kutajwa kwa jina lake na kumlazimu arudi na kuwasili pale alipoitwa bila kusubiri siku iliyopangwa ya kukutana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Askofu Gwajima amesema kuwa kuhusu mali anazomiliki ni kutokana na kazi anazofanya ikiwa kuwa na kampuni mbalimbali pamoja na kufundisha masuala ya farsasafa nje nchi na kulipwa dola za kimarekani 1000 kwa saa.

Aidha amesema kuwa kulindwa kwake ni kutokana na kuwa na usalama wake hata papa ana gari ambayo haipiti risasi wakati ni mtakatifu.

Askofu Gwajima amesema Makonda anachuki na wivu dhidi yake ndio maana anamhusisha na jambo ovu ambalo linamchafu mbele ya mungu.
Amesema kuwa yuko radhi kukaa ndani miaka 40 kutokana na kupigania suala la uovu ni jambo halitawe za kuvumiliwa.
 
Katibu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Gwandu Mwangasa akizungumza na waandishi wa habari juu watavyopambana na katika kupigania Askofu wake Josephat Gwajima leo jijini Dar es Salaam.
Asikofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josepahat Gwajima akitoka katika mkuna na kuelekea kituo Kikuu cha polisi leo jijini Dar es Salaam.
Asikofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josepahat Gwajima akiagana na waumini wa kanisa hilo leo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.