Habari za Punde

BONDIA MOHAMED MATUMLA AFANYIWA UPASUAJI WA KICHWA MOI

Bondia Mohamed Matumla amefanyiwa upasuaji wa kichwa lro mchana baada ya kupigwa ngumi ya kichwa iliyosababisha madhala wakati wa pambano lake lililofanyika jana usiku kwenye Ukumbi wa Uwanja wa ndani wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Baada ya kufikishwa Hospitalini hapoa Matumla alipimwa na Vipimo vya CT scan vikaonyesha kuvuja kwa damu iliyojikusanya sehemu moja na madaktari walianza jitihada za kunusuru maisha ya mwanamasumbwi huyo ambaye hali yake haikuwa nzuri.
Aidha upasuaji huo ulichelewa kufanyika mapema kwa kuwa alihitajika kuongezewa damu, baada ya kuonekana kuvujwa na damu nyingi .

Matumla alifanikiwa kupata damu kutoka chumba cha upasuaji.
Hadi jioni hii hali ya Bondia huyo ilikuwa ikiendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji japo alikuwa bado hajaanza kuzungumza.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.