Habari za Punde

CAMEROON BINGWA KOMBE LA AFCON 2017 YAICHAPA MISRI 2-1


Timu ya Cameroon ya safari hii ilikuwa mbovu katika historia.
Angalau ndivyo walivyoonekana wiki mbili na nusu zilizopita, lakini mpira unadunda. 
Lolote laweza kutokea. Na baada ya wachezaji nyota wanane kujitoa kutokana na kocha wao Hugo Broos kusisitiza nidhamu, majina mengine makubwa yakawekwa benchi. 
Lakini kikosi chake kilichokuwa na uzoefu mdogo kilifanya makubwa na hata kuweza kusawazisha na hatimaye kuishinda Misri kuipanchi hiyo ushindi wa mara ya tano wa kombe hilo la AFCON, na kwanza katika kipindi cha miaka 15.
Majina makubwa ndiyo yaliyorejea uwanjani na kuwezesha ushindi huo, magoli yote yakiwa yamefungwa na wachezaji wa akiba. 
Mohamed Elneny aliipatia Misri bao la kuongoza katika kipindi cha kwanza lakini Nicola Nkoulou alisawazisha kabla bao la ushindi kuwekwa kimiani na Vincent Aboubakar zikiwa zimesalia dakika mbili mchezo umalizike. 
Hakika lilikuwa goli tamu.
Msisimko ulikuwa mkubwa mno uwanjani wakati raia wa Cameroon wanaoishi Gabon walipojitokeza kwa maelfu kushangilia vijana wao, huku mabasi kibao yaliyosafiri usiku kucha kutoka Doula na Yaounde yakileta mashabiki zaidi, na kwa mara ya kwanza uwanja wa L'Amitie ulifurika kwa mara ya kwanza.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.