Habari za Punde

CHELSEA YAZIDI KUWASHA TAA LIGI KUU ENGLAND YAICHAPA ARSENAL 3-1

Mesut Ozil akipiga mpira wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya England leo dhidi ya Chelsea katika Uwanja wa Stamford Bridge mjini London. Katika mchezo huo Chelsea imeshinda mabao 3-1.
***************************************
MASHABIKI wa Washika bunduki leo tena wamezidi kupoteza matumani ya kutwaa taji la Ligi Kuu ya England baada ya kupoteza tena mchezo wa leo dhidi ya Chelsea kwa kuchapwa mabao 3-1.
Chelsea wanaendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi kwa tofauti ya pointi 12 dhidi ya Arsenal yenye pointi 47 na hivyo kufuta matumaini ya kushinda taji hilo walilolitwaa kwa mara ya mwisho mwaka 2004.

Kwenye mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Stamford Bridge Chelsea walitangulia kufunga kwa bao la beki wa kushoto Marcos Alonso kwenye dakika ya 13.
Alonso alifunga bao hilo kwa kichwa baada ya kumzidi nguvu beki wa kulia wa Arsenal Hector Bellerin aliyeumia katika harakati za kutaka kuokoa.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.