Habari za Punde

SERIKALI YAFAFANUA MIKOPO KWA VIJANA


Serikali imetoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa mikopo kwa vijana na malipo ya ada kwa fedha za kigeni. Ufafanuzi huo umetolewa mjini hapa leo wakati wa kikao cha pili katika Mkutano wa Sita wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Kuwainua Vijana Kiuchumi.

Akijibu hoja kuhusu namna vijana kutoka sehemu mbalimbali nchini wanavyoweza kufaidika kiuchumi, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira), Anthony Mavunde, amesema Serikali imetenga fedha za kutosha kupitia mifuko mbalimbali kuwawezesha vijana kwa mitaji na mafunzo ya ujasiriamali ili kuwainua kiuchumi.
Ameongeza kuwa vijana wenyewe ndio wanaopaswa kuchangamkia fursa hizo na pale wanapojiunga katika vikundi mbalimbali wamekuwa wakipewa mikopo kwa ajili ya mitaji. Alitoa mfano wa jinsi Serikali ilivyowawezesha vijana waliojiunga na kuwekeza katika viwanda vidogo vya maziwa na chaki mkoani Simiyu.
Amewataka pia Wabunge na Halmashauri zote nchini kuendelea kupigania kutengwa maeneo maalum katika sekta mbalimbali kwa ajili ya kuwapatia vijana na kutengwa kwa asilimia 5 ya mapato ya Halmashauri kwa maendeleo ya vijana.

SI TATIZO KUTUMIA MAJENGO YA UDOM

Serikali imesisitiza kuwa baadhi ya Wizara zilizoanza kutekeleza agizo la kuhamia Dodoma kutumia baadhi ya majengo kwa muda kwenye Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) hakutaathiri shughuli za chuo.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama. Waziri Jenista amesisitiza kuwa baadhi ya Wizara zitatumia majengo ya UDOM kwa sababu mengi ya majengo hayo yalikuwa hayatumiki kwa sasa kwa shughuli za chuo hicho na hakutakuwa na muingiliano na shughuli za chuo.


MRADI WAMABILIONI MAJI DAR
Serikali kwa kushirikiana na Mamlaka ya Maji Dar es Salaam imeanza kutekeleza mradi wa usambazaji wa maji utakaogharimu Dola za Marekani milioni 32.772 ambazo ni mkopo kutoka Benki ya Exim ya China. Mradi huo utahusisha sehemu yote ya jimbo la Kawe, Dar es Salaam. Mradi huo utachukua miezi 15.

Imetolewa na:
Idara ya Habari-MAELEZO.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.