Habari za Punde

GARI LA MAFUTA LAKAMATWA MKOANI NJOMBE LIKIWA LIMEJAZA VIPODOZI FEKI

 Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Ole Sendeka, akionyesha baadhi ya Vipodozi Feki vilivyokamatwa kwenye Gari la Mafuta vilivyokuwa vikisafirishwa jana.

Gari hilo lililokuwa na shehena hiyo ya Vipodozi.
*********************************************************
JESHI la Polisi Mkoani Njombe , limekamata magari mawili ya kubeba Mafuta yakiwa yamebeba Vipodozi hatari kwa matumizi ya binadamu, vyenye uzito wa Tani 10.     
Baada ya tukio hilo Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka, amemwagiza Makamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe,kushirikiana na TRA,TAKUKURU , TFDA na Wakala wa Barabara (TANROARD) kufutilia vipondozi hivyo vimeingiaje Nchini na kuvuka mpaka kutoka Tunduma, Songwe, Mbeya hadi kukamatiwa Mzani wa Makambako.   Mpaka sasa watu watatu wanashikiliwa na Jeshi la polisi kulisaidia Jeshi la Polisi juu ya tukiohilo.
 Sehemu ya Maboksi yenye Vipodozi hivyo  
Vijana wakishusha maboksi yenye Vipodozi hivyo kutoka ndani ya gari hilo la mafuta,ambalo lilijazwa mzigo wa vipodozi badala ya mafuta.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.