Habari za Punde

HATMA YA KESI YA MAUAJI YA MKE WA BILIONEA MSUYA MWEZI UJAO.

Mke wa aliyekuwa Bilionea Erasto Msuya na mwenzake Revocatus Muyela wakiwa mahakamani wakisubiri kusomewa mashtaka yao mapya ya mauaji baada ya Jana kuachiwa huru na kisha kukamatwa tena. 
Mrita na mwenzake wanatuhumiwa kumuua kwa kukusudia Aneth Msuya ambaye ni Dada wa Marehemu wa Bilionea Msuya 
Washtakiwa hao wakijadili jambo na wakili wao Peter Kibatala(wa pili kutoka kushoto).
*************************************************
Wakili wa utetezi, katika kesi ya mauaji ya inayomkabili mke wa marehemu bilionea Erasto Msuya, Miriam Mrita, Peter Kibatala ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa haina mamlala ya kisikiliza kesi hiyo kwa kuwa washtakiwa walishaachiwa huru.Kibatala amedia kuwa kitendo cha Mahakama hiyo kusikiliza kesi ambayo Jana watuhumiwa waliachiwa huru ni sawa na kuichonganisha Mahakama na kufanya maamuzi ya Hakimu aliyewaachia huru kuonekana hapana maana. 
Jana, Hakimu Mkazi Godfrey Mwambapa wa Mahakama hiyo aliwachia huru Mrita anayeshtakiwa pamoja na Revocatus Muyela baada ya upande wa mashtaka kushindwa kutekeleza amri ya mahakama iliyowataka kurekebisha hati ya mashtaka kwa kuwa inamapungufu.Hata hivyo, washtakiwa hao walikamatwa tena jana hiyo hiyo na jeshi la polisi na kisha Leo asubuhi wamepandishwa mahakamani hapo kusomewa upya tuhuma za mauaji ya Aneth. 
Katika kesi hiyo, mshtakiwa Mrita anadaiwa kumuua wifi yake Aneth Msuya akishirikiana na Revocatus Muyela.Inadaiwa kuwa mauaji hayo yalifanyika Mei 25, mwaka Jana huko Kibada Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam. 
Mata baada ya kusomewa tuhuma hizo za mauaji, washtakiwa hawakutakiwa kujibu kitu kwa kuwa Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji ambazo zinasikilizwa Mahakama Kuu.
Kabla upande wa jamuhuri haujasoma kesi hiyo Wakili Kibatala aliiomba mahakama kutoyasikiliza mashtaka hayo kwa kuwa Kisutu haina mamlaka. 
Lakini Hakimu Thomas Simba aliwaamuru upande wa mashtaka kuisoma kwanza kesi hiyo ndipo awasikilize hoja zao.Mara baada ya kusomewa tuhuma zao na kutotakiwa kujibu kitu, ndipo Kibatala alipoibuka na hoja hizo ambazo zilipingwa na upande wa Jamuhuri.Akijibu Hoja hizo, wakili wa serikali mkuu, Mutalemwa Kishenyi alidai kuwa uamuzi wa Hakimu Mwambapa kuwaachia huru washtakiwa hao uliishia hapo hapo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.