Habari za Punde

KIPA WA KAGERA SUGAR MAREHEMU DAVID BURHAN AZIKWA IRINGA LEO

Mkurugenzi wa Uanachama wa TFF, Eliud Mvella ambae alimwakilisha Rais wa TFF , Jamal Malinzi katika kutoa salam za TFF kulia ni meneja wa uendeshaji mwakilishi wa bodi ya ligi Fatma Abdallah Shibu.
Waombolezaji wakiwa katika uwanja wa Samora.
Mwili wa marehemu David ukitolewa kwenye gari.
Wachezaji wa Kagera Sugar wakiaga mwili wa mwenzao.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Mtangazaji wa radio Ebony FM ya Iringa Eddo Bashir (mwenye kofia nyekundu kushoto ) akishiriki kubeba mwili wa David.
Baadhi ya viongozi wa chama cha soka mkoa wa Iringa ,viongozi wa siasa na dini wakiwa jukwaaa kuu
Wawakilishi wa timu ya Mbeya City waliofika kushiriki mazishi kutoka Mbeya.
Msemaji wa Lipuli Fc Clement Sanga akiongoza wanahabari Iringa kutoa heshima za mwishi kwa David Burhan.
Mwanahabari wa TBC Iren Mwakalinga na Zuhura wa Azam TV na wanahabari wengine wakitoa heshima za mwisho.
Mwanahabari wa Ebony FM Sport Bw Stev akiaga mwili.
Mwanahabari wa Mwananchi Iringa Godfrey Nyang'oro.
Kingozi wa timu ya African Wanderers Shukuru Lwambati akitoa heshima za mwisho.
Mchezaji wa zamani wa Costa Magoroso akitoa heshima za mwisho
Mamia ya waombolezaji wakisubiri kuaga mwili uwanja wa samora
Na Mwandishi Wetu, Iringa 
UONGOZI wa shirikisho la chama cha mpira wa miguu nchini (TFF) umeongoza mamia ya wakazi wa mkoawa Mbeya ,Kagera na Iringa katika mazishi ya aliyekuwa mlinda mlango wa timu ya Kagera Sugar David Burhan ,huku uongozi wa Kagera Sugar na Lipuli Fc wakiahidi kucheza mechi ya kirafiki Februari 11 uwanja wa Samora kwa ajili ya kuichangia familia yamarehemu Burhan 

Akizungumza leo katika uwanja wa Samora wakati akitoa salam kabla ya kuaga mwili huo wa Burhan kwa mazishiyaliyofanyika makaburi ya makanyagiomjini Iringa mkurugenzi wa Uanachama wa TFF, Eliud Mvella ambae alimwakilisha Rais wa TFF , Jamal Malinzi alisema kuwaTFF amepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha mlinda mlango huyo waKagera Sugar hasa ukizingatia kwa msimu uliopita ndie alikuwa mlinda mlango bora akitokea timu ya Mbeya City“.
Kwa niaba ya Rais wa TFF JamaliMalinzi nimefika kumuwakilisha ila anawapa pole sana timu yamaji maji ,Mbeya City , Lipuli Fc pamoja na timu ya Kagera Sugar ambayo ndio amekuwa akiichezea hadi kifo kinamkuta ….kwa kuondokewa namchezaji huyo iwe chachu kwa wanamichezo wote kuongeza bidii katika michezo na kuzidi kusonga mbele zaidi”

Alisema kuwa TFF itaendelea kushirikiana na familia hadi pale msiba huo utakapomalizika na hivyo TFF pamoja na bodi ya ligi ,bodi ya lingi ukizingatia ndio ambao walisimamia lingi nzima wanatoa rambi rambi ya Tsh 500,000 na TFF Tsh 500,000“ 
Baaada ya kusema hayo naomba tumsindikize ndugu yetu salama naukizingatia mimi nilikuwepo hapa na hata tunapohangaika kuipandisha LipuliFc mwaka jana na miaka minginemarehemu alitoa mchango mkubwa sana hata kabla sijaenda TFF hivyo naomba tumuenzi kwa kuiwezesha timu ya Lipuli Fc ambayo inatarajia kupanda daraja iwe ni sehemu ya kumuenzi Burhan “ 
Kwa upande wake msemaji mkuu wa timu ya Kagera Sugar Mohamed Husein alisema kuwa timu yake imempoteza mmoja kati ya walinda mlango wazuri na kuwa timu hiyo pamoja na kushika nafasi ya tatu katika msimamo wa lingi ya VPL bado inaendelea kucheza huku ikiwa na pengo kubwa kwa kuwa na walinda mlango wawili pekee jambo ambalo nihatari kwa timu yake kufanya vizuri .
Kwani alisema hadi sasa timu hiyoimebaki na walinda mlango wawili pekee baada ya kifo cha Burhan na kuwa wataendelea na mchakato wa kuzibapengo hilo japo hawana hakika wa kumpatamrithi atakayefanana na marehemu huyo .
Msemaji huyo alisema kwa ajili ya kumuenzi mlinda mlango wao wamekusudia Februari 10 kuondoka Kagera kuja mkoani Iringa kwa ajili ya kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Lipuli Fc katika uwanja wa Samora kwa ajili ya kutoa ahsante kwafamilia ya marehemu huyo kwa mchango wake kwa timu ya Kagera Sugar na Lipuli FC ,mchezo utakaochezwa siku ya tarehe 11 na kiingilio chotekitaelekezwa kwa familia ya marehemu huyo.

Msemaji wa Lipuli FC Clement Sanga alisema kuwa pengo la Bruah ni vingumu kuzibika kwani hadi hapa ilipo timu yake yaLipuli Fc ni mchango wa marehemuhuyo ambaye alijitolea kwa ajili ya kuona Lipuli Fc inafanya vema . Katika msiba huo mashabiki na wachezaji wa timu ya Mbeya City waliweza kushiriki pia timu za Panama Girls Fc , viongozi wa timu ya Maji maji na 
viongozi wengine wengi walipata kushiriki kutoa salama zao.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya familiailiyosomwa na mmoja kati ya familia JohnMelele alisema Marehemu David Burhan alizaliwa tarehe 25 /1 / 1989 katika Hospitali ya Taifa ya Mhimbili alianzashule ya msingi Wilolesi Iringa mjini 1994-2000baada ya kumaliza elimu ya msingi aliweza kujiunga na timu za mpira wa miguu mbali mbali na kuwa kifo chake kimetokana na ugonjwa wa ini

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.