Habari za Punde

KIWANDA CHA KOBIL CHAAMULIWA KUBOMOA JENGO LAKE,MAMLAKA YA UENDELEZAJI KANDA MAALUM ZA KIUCHUMI (EPZA) NA KIWANDA CHA TOOKU VYATOZWA FAINI YA MIL.30 KW

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina akiangalia suruali aina ya Jinsi  zinazozalishwa katika kiwanda cha EPZ wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa mazingira mapema hii leo Jijini Dar es salaam.
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina akiwa katika ziara ya ukaguzi wa Mazingira katika kiwanda cha uwekezaji cha EPZ, kilichopo Terminal Jijini Dar es salaam.     
. Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina akiangalia shughuli za uzalishaji wa nguo katika kiwanda cha nguo cha EPZ mara baada ya kufanya ziara ya ukaguzi wa mazingira katika kiwanda hicho kilichopo Ubungo Terminal Jijini Dar es salaam. 
****************************************************


SERIKALI imetoa siku 30 kwa Kiwanda cha KOBIL kilichopo 

maeneo ya Keko kuvunja jengo lake lililojengwa juu ya mtaro wa 

kupitishia maji ya mvua na kusababisha maji hayo kutopita 

vizuri.
Akitoa agizo hilo Jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Nchi 

Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira na Muungano,Luhaga Mpina 

amesema mnamo Februari 15 mwaka huu,alifanya ukaguzi katika 

eneo la Keko na kutoa maelekezo kwa kiwanda cha Kobil kumpatia 

taarifa juu ya nyaraka zao zilizowahararishia kujenga jengo 

lao juu ya mtaro huo.
Amesema alipitia taarifa za kiwanda hicho cha kobil Tanzania 

na kujiridhisha nayo kuwa hakuna kibari chochote kilichotolewa 

dhidi ya kiwanda hicho kujenga juu ya mtaro huo.
Mpina amesema kujenga jengo juu ya mtaro au mfereji wa maji ya 

mvua ni kinyume cha sheria ya Mazingira namba 20 ya mwaka 

2004,Sheria ya ardhi namba 4 ya mwaka 1999 ambapo pia ni 

kinyume cha sheria ya mpango mji ya mwaka 2007.


"Februari 15 mwaka huu,nilifanya ukaguzi katika eneo la Keko 

ambapo baadhi ya viwanda viwili vilijengwa juu ya mtaro wa 

maji ya mvua na kusababisha kero kwa wananchi wa eneo hilo 

pale mvua zinaponyesha,hivyo nilitoa agizo ya kiwanda cha 

Redsea kubomoa jengo lake ndani ya siku 30 na leo natoa agizo 

kwa Kobil kubomoa jengo lao ndani ya siku hizo,"amesema
Aidha amesema kuwa Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira (NEMC) 

liwaandikie hati ya siku 30 Kampuni hiyo ya Kobil kubomoa 

wenyewe jengo lao na endapo hawatabomoa serikali itabomoa kwa 

gharama zao wenyewe.


Mpina ameseama viwanda hivyo vimejengwa juu ya mtaro ambapo 

mvua kubwa ikinyesha maji ya mvua hayo yanashindwa kupita 

vizuri na kusababisha mafuriko makubwa kwa wananchi.

Ameongeza kuwa Kobil inatakiwa kubomoa jengo lao ili kupisha 

mfereji huo wa maji ya mvua kuongeza kasi ya maji ya mvua 

pindi mvua inaponyeshwa. 
"Tumejiridhisha vya kutosha kwamba hakuna upepembuzi yakinifu 

uliofanyika katika majengo haya wakati wa majengo haya 

yalipokuwa yanajengwa,"amesema Mpina.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.