Habari za Punde

SIMBA WAWAKALISHA TENA YANGA NI KICHUYA TENA ALIYEZAMISHA JAHAZI, SIASA ZAHAMIA KWENYE SOKA


Kichuya akishangilia na mashabiki baada ya mpira kumalizika na kuibuka kedede kwa ushindi wa mabao 2-1. Bao la Yanga lilifungwa kwa mkwaju wa penati na Simon Msuva katika dakika ya 7, bao la kuswazisha la Simba lilifungwa na Loudit Mavugo dakika ya 66 na bao la ushindi lilifungwa na Shiza Kichuya katika dakika ta 80.
Mgombea Urais wa mwaka 2015 kupitia CHADEMA Edward Lowassa, akisimama na kupunga mkono kuwasalimia mashabiki wa soka baada ya kuwasili uwanjani hapo kushuhudia mtanange wa Simba na Yanga jioni ya leo.
 Shabiki wa Simba akiwa na bendera ya CHADEMA huku akishangilia wakati wa mtanange huo jambo ambalo ni tofauti na soka na ni adimu kuona vitu kama hivi katika soka hususan uwanjani na katika mechi kubwa kama hiyi.

Kabla ya kuanza kwa mtanange huo walionekana mashabiki wa Simba na Yanga wakiungana ambapo wa Yanga walitoka upande wao wakiwa na sare zao na kwenda upande wa Simba na kukumbatiana na kuonyesha alama ya vidole viwili huku wakishangilia na kuwashangaza baadhi ya wengine waliokuwapo uwanjani hapo.


 Penaaaaaati.....Obrey Chirwa akiangushwa ndani ya boksi

Kipa wa Simba Daniel Agyei, akijaribuku kuruka kupangua mpira wa penati uliopigwa na Simon Msuva katika dakika ya 7.

Simon Msuva akikimbia kushangilia bao lake
Obrey Chirwa akijianda kupiga shuti.
 Simon Msuva (kulia ) akichuana kuwania mpira na Mohamed Hussein.
 Amis Tambwe akichuana na


 Chirwa akituliza mpira katikati ya msitu wa mabeki
 Wachezaji wa Simba wakishangili bao la kwanza
 Kaseke akimtoka Said Ndemla
 Kichuya na wenzake wakishangilia bao la pili
 Kipa wa Simba Agyei akishangilia bao la pili
 Askari wakimbeba shabiki wa Simba aliyezimia uwanjani

 Makocha wa Simba wakipongezana baada ya kuibuka kidedea.

 Mashabiki wa Simba wakishangilia ushindi    
.Mashabiki wa Yanga wakiwa hoi.....
Simon Msuva akikimbia kushangilia bao lake
Msuva akishangilia bao lake

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.