Habari za Punde

LIGI KUU YA WANAWAKE SASA RASMI KUANZA FEBRUARI 26

Ligi Kuu ya Wanawake ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) hatua ya 6 Bora itaanza rasmi Februari 26, 2017 kwenye kituo kimoja cha Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala, Dar es Salaam.
Timu sita zilizofanikiwa kufika hatua ya Sita Bora ni JKT Queens ya Dar es Salaam, Mlandizi Queens ya Pwani na Fair Play ya Tanga kutoka Kundi “A” wakati kutoka Kundi “B” zimo Marsh Acedemy ya Mwanza, Sisterz ya Kigoma na Panama ya Iringa.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo, kutakuwa na mechi mbili kila siku katika kituo kimoja kwa mujibu wa kanuni. Kituo hicho ni Uwanja wa Karume, ulioko Ilala jijini Dar es Salaam ambako mchezo wa kwanza utaanza saa 8.00 mchana wakati mwingine utaanza saa 10.00 jioni.
Ratiba mpya inaonesha kwamba siku ya Februari 26, mwaka huu kutakuwa na mchezo kati ya JKT Queens na Mlandizi saa 8.00 mchana wakati saa 10.00 kutakuwa na mchezo kati ya Fair Play na Sisterz.
Ratiba kamili kwa mechi inazofuata itatolewa wiki ijayo. Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza au unaoweza kujitokeza kutokana na mabadiliko hayo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.