Habari za Punde

MAMA MAGUFULI NA MAMA MAJALIWA WAWAOMBA WANANCHI WASAIDIE WATU WASIOJIWEZA

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakiwakabidhi mafuta maalumu wawakilishi wa wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi walioalikwa kwenye hafla iliyofanyika katika kituo cha wazee na watu walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma cha Amani Ipuli katika Manispaa ya Tabora mkoani Tabora leo.
*************************************
MKE wa Rais Mheshimiwa Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wametoa wito kwa Watanzania kujengea utamaduni wa kutembelea vituo vya wazee na watu wenye mahitaji maalumu na kutoa misaada ili waweze kujikimu.
Wameyasema hayo leo (Jumatano, Februari 15, 2017) wakati walipotembelea Makazi ya Wazee wasiojiweza na walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma ya Amani Ipuli yaliyoko kwenye Manispaa ya Tabora mkoni Tabora.
Katika makazi hayo wamekabidhi tani 7.5 za vyakula mbalimbali ukiwemo mchele, unga wa sembe na maharage pamoja na mafuta maalumu kwa ajili ya watoto wenye ulemavu wa ngozi wanaosoma katika shule mbalimbali mkoni Tabora.
Hata hivyo, Mama Janeth amewapongeza watumishi wote wanaofanyakazi kwenye makazi ya kulelea wazee na watu wenye mahitaji maalumu kwa sababu kazi hiyo ni ngumu na ina changamoto nyingi.“Ibada si kwenda katika nyumba za ibada pekee bali hata kuwatembelea wazee, watu wenye mahitaji maalumu na wasiojiweza utakuwa umetoa sadaka kubwa kwa Mwenyezi Mungu. Nawaomba tujitahidi kuwatembelea,” amesema.
Kwa upande wake Mama Mary amewaomba wananchi wote wawe na utaratibu wa kuwasaidia wazee wanaoishi katika makaazi ya kulele wazee, walemavu na wasiojiweza nchini na kuwafariji kwa sababu wanahitaji upendo na faraja kutoka kwao.
Pia Mama Mary ameipongeza Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na wadau mbalimbali kwa kujitoa kwa hali mali katika kuwahudumia wazee na watu wenye mahitaji maalumu.Naye Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala amesema Serikali itahakikisha huduma zinaboreshwa katika makazi ya kulelea wazee na watu wenye mahitaji maalumu nchini kwa kuwa vingi viko katika hali mbaya.
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakikabidhi sehemu ya msaada wao wa tani 7.5 ya vyakula katika kituo cha wazee na watu walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma cha Amani Ipuli katika Manispaa ya Tabora mkoani Tabora leo Februari 15, 2017
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakiongea na mmoja ya wazee wasiojiweza wanaolelewa katika kituo cha wazee na watu walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma cha Amani Ipuli katika Manispaa ya Tabora mkoani Tabora leo Februari 15, 2017
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakiongea na mmoja ya wazee wasiojiweza wanaolelewa katika kituo cha wazee na watu walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma cha Amani Ipuli katika Manispaa ya Tabora mkoani Tabora leo Februari 15, 2017
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wakilakiwa kwa nderemo walipowasili katika kituo cha wazee na watu walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma cha Amani Ipuli katika Manispaa ya Tabora mkoani Tabora leo Februari 15, 2017
Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa akisalimia wananchi na wazee wasiojiweza wanaolelewa katika kituo cha wazee na watu walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma cha Amani Ipuli katika Manispaa ya Tabora mkoani Tabora leo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.