Habari za Punde

MANJI KUTEKELEZA AGIZO LA MAKONDA, AAHIDI KUFIKA KITUONI KESHO ASUBUHI


 BAADA ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paulmakonda leo kutangaza jumla ya majina 65 ya watu aliowataka kufika Kituo vha Posili Kati, siku ya Ijumaa akiwemo Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, yeye amejipanga kutekeleza agizo hilo siku ya kesho kwenda kuripoti Central Police badaya ya keshokutwa, ili kupunguza msongamano wa idadi ya watu waliotajwa.

Mkuu wa Mkoa wa Polisi wa Dar es Salaam ametaja majina hayo leo ambapo watu hao wanatakiwa kufika Kituoni hapo kwa ajili ya kutoa msaada kwa serikali kuhusiana na matumizi Sakata la dawa za kulevya linaloendelea nchini kwa hivi sasa.


Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, leo jioni Manji alisema kuwa  hawezi kubadili ratiba zake kwa keshokutwa na kwenda kupanga foleni ya watu 65 kwa ajili ya kitu hicho na badala yake atakwenda kesho ili kupunguza msongamano huo na kesho kutwa aweze kuendelea na ratiba zake.
Aidha Manji alisema, kwa siku iliyotajwa tayari alishakuwa na ratiba za kazi zake binafsi na kuahidi kutekeleza agizo hilo la Serikali kupitia kwa Mkuu wa Mkoa, kesho asubuhi na mapema.

''Sijakataa kwenda Kituoni kama alivyotangaza Mkuu wa Mkoa,ila nitajitahidi nifike siku ya kesho asubuhi na mapema na baada ya shughuli niliyoitiwa na mimi nitaanza mchakato wa kwenda mahamakani kwa ajili ya kumfungulia mashtaka Makonda kwa kunidharirisha, kwa kutumia vibaya jina langu, kwani kitendo cha kutumia jina la MTU vibaya ni makosa na katiba ya nchi inaniruhusu kumshtaki Makonda," alisema Manji.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.