Habari za Punde

MARTIN KADINDA NA MARAFIKI WA WEMA WASOTA MAHAKAMANI, KADINDA AMKANA WEMA KUWA SI MENEJA WAKE KWA SASA

Aliyekuwa meneja wa wema Martin Kadinda akiwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam pamoja na wanasheria
Baadhi ya marafiki wa Wema Spetu wakiwa wamesimama kusubiri msanii huyo kuletwa mahakamani
Jike Shupa na wenzie wakiwa wamekata tamaa mara baada ya kuambiwa Wema haletwi mahakamani
**************************************************
Na Mwandishi Wetu, Dar
Mbunifu wa mitindo maarufiu nchini, Martin Kadinda amesema kuwa yeye sio meneja wa msanii Wema Sepetu kwa sasa bali amefika mahakamani hapo kama rafiki wa karibu wa msanii huyo.

Kadinda amesema hayo katika maongezi maalum na mwandishi huyu juu ya uhusiano wake na Wema Sepetu kwa sasa hasa mara baada ya kuhusishwa na tuhuma za matumizi na uuzwaji wa dawa za kulevya.

“Kwa sasa mie sio meneja wa Wema.K wa sasa mimi ni rafiki yangu tu wa karibu hivyo nimeamua kuja hapa kwa ajili ya kujua rafiki yangu amefikia wapi katika kipindi hiki ambacho anapitia magumu” amesema Kadinda

Amesema kuwa yeye kwa sasa anaendelea na biashara yake ya kushona suti tu hili aweze kujipatia ugali wake wa kila siku na sio kujihusisha na makundi ambayo sio sahihi.

Kadinda na marafiki kadhaa wa Wema wameonekana mahakamani hapo wakisubiri kwa hamu kumuona rafiki yao anafikishwa hapo lakini hakufikishwa kama ilivyoelezwa awali.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.