Habari za Punde

MASOGANGE NAYE ADAKWA KWA TUHUMA ZA DAWA ZA KULEVYA

TAARIFA zilizotufikia, zinaeleza kwamba Video Queen maarufu Tanzania, Agness Gerald almaarufu "Masogange", anashikiliwa na Jeshi la Polisi, Kituo Kikuu (Central) akituhumiwa kuhusika na biashara na matumizi ya madawa ya kulevya.
Masogange alikamatwa na Polisi jana usiku na taarifa zinaeleza kwamba mpaka sasa bado anashikiliwa central.
Mwanadada huyo anaingia kwenye orodha ya wasanii wengine na watu maarufu nchini, walioshikiliwa na wanaoendelea kushikiliwa wakihusishhwa na sakata la matumizi na biashara ya Dawa za Kulevya, katika vita kali inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Taarifa zaidi kuhusu kukamatwa kwa Masogange zitafuatia...
Masogange alikamatwa na polisi jana usiku na taarifa zinaeleza kwamba, mpaka muda huu bado anashikiliwa Kituo Kikuu cha Polisi Kati (Central).

Taarifa zaidi kuhusu kukamatwa kwa Masogange na kinachoendelea, zitaendelea kukujia kupitia hapahapa, endelea kufuatilia mtandao huu na pia kufuatilia Global TV Online.  Source: Global Publisher

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.