Habari za Punde

MAWAZIRI 15 WA NCHI ZA SADC KUKUTANA DAR KESHO JIJINI DAR

Na. Immaculate Makilika- MAELEZO
Mawaziri 15 wa Nchi  Wananchama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika ( SADC), wanatarajia kufanya mazungumzo kesho jijini Dar es salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiao wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga alisema kuwa mawaziri hao wanatarajiwa kuzungumza masuala mbalimbali ikiwemo elimu, ushiriki wanchi za SADC, ikiwa ni pamoja na kuzungumzia haliinayoendelea nchini Msumbiji.
“Tanzani ni  mwenyeji na wenyekiti wa Mkutano huo, ambapo pia inaongoza Kitengo Maalumu cha Masuala ya Ulinzi,Usalama pamoja na Siasa, pia kamati ya siasa na diplomasia inatarajiwa kukutana pia wiki hii” alisema Waziri Mahiga.
Kila mwaka mawaziri hao hukutana mara moja, kwa lengo la kuzungumzia masuala  mbalimbali yanayohusu nchi wanachama wa umoja huo.
Katika hatua nyingine,  Waziri Mahiga alisema kuwa ,Tanzania  inashirikiana na  Msumbiji kufanyia kazi suala la  watanzania walihamishwa nchini.
“ Hili ni zuala gumu kidogo tusitoe majibu rahisi, na hivyo Serikali zote mbili zinaendelea kufanya mazungumzo zaidi juu ya suala hili” alisema Waziri Mahiga.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.