Habari za Punde

MBEYA CITY KAMILI KUWAVAA MWADUI FC KESHO


KIKOSI cha Mbeya City Fc kimefanya mazoezi ya mwisho asubuhi ya leo kwenye uwanja wa shule ya sekondari ya Kom mjini Shinyanga tayari kwa mchezo wa ligi kuu ya vodacom Tanzania bara dhidi ya Mwadui Fc uliopangwa kuchezwa kesho Mwadui Complex.
Akizungumza na mbeyacityfc.com mapema leo, Ofisa habari wa kikosi hiki, Dismas Ten amesema maandalizi yote kwa ajili ya mchezo huo yamekamilika asilimia mia moja,hasa baada ya program za mazoezi kufanyika kwa siku mbili kama ilivyokuwa imeelekezwa na kocha Kinnah Phiri na kinachosubiriwa sasa ni dakika 90 za mchezo wa kesho.
Tumekuwa na siku mbili nzuri za mazoezi tangu tulipofika hapa Shinyanga siku ya juzi, tumekamilisha maandalizi yote tunasubiri dakika 90 za kesho, tunafahamu Mwadui ni timu nzuri lakini matokeo huja kulingana na vile ambavyo umejiandaa, sisi tumejiandaa vizuri kuhakikisha tunashinda mchezo ili kupata pointi tatu, lengo letu ni kuona tunakuwa sehemu ya timu nne za juu mwisho wa msimu.
Akiendelea zaidi Ten alisema nyota wote 20 walisafiri kwaa ajili ya michezo miwili ya kanda ya ziwa wako kwenye hali nzuri pasipo majeraha yoyote kwa mujibu wa taarifa ya daktari, na hakuna shaka kuwa wako tayari kuitetea timu yao kwa uhakika na nguvu zote.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.