Habari za Punde

MCHEZO WA MARUDIANO WA YANGA NA NGAYA KUPIGWA KESHO, TFF YAWAONYA WABEBA MABANGO KESHO

Maandalizi ya mchezo wa kimataifa kati ya Young Africans ya Tanzania na Ng’aya ya Comoro, unaopigwa kesho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, yamekamilika kwa asilimia 100.

Timu ya Ngaya tayari imeshawasili Dar es Salaam, ambako Young Africans wao wameweka kambi kwenye Hoteli ya Zimbo iliyoko Kariakoo kwenye makutano ya mitaa ya Ndovu na Nyamwezi, Dar es Salaam.

Kwa upande wa timu ya N’gaya, yenyewe imefikia Hoteli ya Kaluganje iliyoko Mtaa wa Gerezani, Kariakoo wakati waamuzi kutoka Uganda, pamoja na Kamishna wa mchezo wanatarajiwa kutua jijini leo.

Mchezo huo wa marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Young Africans ya Tanzania na Ngaya ya Comoro hatua ya awali utachezeshwa na Waamuzi 
Alex Muhabi Nsulumbi atayekapuliza filimbi uwanjani, akisaidiwa na Ronald Kakenya na Lee Okello wakati Mwamuzi wa Akiba atakuwa Brian Nsubuga Miro,  
kutoka Uganda huku Kamishna wa mchezo huo akitokea Afrika Kusini ambaye ni Monnyenyone Lucas Nhlapo.

Mchezo huo utachezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kama ambavyo Young Africans walithibitisha CAF majuma mawili yaliyopita kabla ya terehe ya mchezo huo ambayo ni Februari 18, mwaka huu.

WAKATI HUO HUO: TFF imetoa onyo kwa baadhi ya watu walioripotiwa kuwa wamejipanga kuingia na mabango uwanjani hapo kwa ajili ya kuikashifu TFF na Serikali, '
''Tumepata taarifa kuwa kuna baadhi ya watu wana mpango wa kuonyesha mabango yenye ujumbe wa kukashifu Serikali na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na wadau wengine,

Tunachukua fursa hii kuonya wanafamilia ya mpira wa miguu wanaotaka kujihusisha na mipango hiyo, kuacha mara moja kwani vyombo vya dola vitakuwa makini kuangalia aina yoyote ya utovu wa nidhamu uwanjani''. alisema msemaji wa TFF Alfred Lucas

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.