Habari za Punde

MKUTANO WA BARAZA KUU LA BODI YA LIGI KUFANYIKA FEBRUARI 26, 2017

Mkutano wa Tatu wa Baraza Kuu la Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) chini ya Mwenyekiti wake Bw. Hamad Yahya Juma utafanyika Jumapili, Februari 26 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Wajumbe wa Mkutano huo wa mwaka 2016 ambao utaanza saa 4 asubuhi ni wenyeviti wa klabu zote za Ligi Kuu ya Vodacom, na klabu zote za Ligi Daraja la Kwanza.
Ajenda za Mkutano huo ambazo zimeainishwa katika Ibara ya 21 ya Kanuni za Uendeshaji Bodi ya Ligi Kuu ni Kuhakiki Akidi, Kufungua Mkutano, Kuthibitisha Ajenda, Kuthibitisha Muhtasari wa Mkutano Uliopita, Yatokanayo na Mkutano Uliopita, Hotuba ya Mwenyekiti, Taarifa ya Utendaji ya Kamati ya Uongozi, Taarifa ya Hesabu zilizokaguliwa, Kupitisha Bajeti, Mengineyo na Kufunga Mkutano

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.