Habari za Punde

MKUU WA MKOA PAUL MAKONDA AWEKA HADHARANI MAJINA YA WAUZA UNGA JIJINI DAR

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akipitia orodha ya majina ya maafisa wa Polisi wanaotuhumiwa kujihusisha na biashara ya madawa za kulevya.
************************************************
Na Mwandishi Wetu Dar.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewataja Askari 9 wanaotuhumiwa kuhusika na biashara ya dawa za kulevya. pamoja na baadhi ya wasanii maarufu nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, Makonda aliwataja jumla ya Askari 9 
na kusema kuwa Serikali ya awamu ya Tano haiko tayari kuvumilia vitendo vya kwenda kinyume na taratibu za nchi kama kuza dawa za kulevya.
Aidha Makonda alitoa agizo kwa jeshi la polisi kuwakamata Maafisa wote wa jeshi la polisi waliotajwa kushirikiana na wauza madawa ya kulevya mpaka pale uchunguzi utakapokamilika.
"Ni mepata taarifa kuwa baadhi ya Askari wa Jeshi polisi wanajihusisha na uuzwaji wa madawa ya kulevya na wengine wamekuwa na utaratibu wa kwenda kuchukua pesa kila jumamosi kwa wauzaji wa madawa hayo na ndio maana biashara hii inaendelea kuwepo kwakuwa wanashirikiana na wauzaji" alisema Makonda.
Wakati huo huo Makonda amewataka wale wote waliotajwa kuhusika na kuuza dawa za kulevya kufika katika kituo cha polisi cha kati (Centre Police) kwa ajili ya mahojiano.
''Kuna maeneo watu wanatuambia madawa ya kulevya wanayapata sehemu hizo, wamiliki wake kesho niwakute polisi, wasipokuja nitawafuata, 
Kama unajua una eneo unafanya biashara za dawa za kulevya hapa jijini Dar es Salaam, natoa siku 7 biashara hii iishe, operesheni hii naiongoza mwenyewe
Kama Kamishna Sirro na timu yake watashindwa kutokomeza dawa za kulevya maana yake wamekosa sifa za kuendelea kuwa askari, 
Watano tayari nimeshawakamata na wengine nimewakamata wakiwa na dawa za kulevya'' alisema RC Makonda

Baadhi ya majina yaliyotajwa ni:- 
1- Detective Koplo Noel (Kituo chake cha kazi ni Central Police Dar)
2- Dotto (Yuko Kituo cha Kijitonyama)
3- Mwingine anafahamika kama 'Makomeo' (Kituo cha Oyster-bay)
4- Glory (Yuko Kituo cha Kawe)
5- Inspector Fadhili (Yuko Kituo cha Kinondoni)
6- Steve (Kinondoni)
7- James (Kinondoni)
8- Ditective Koplo (Wille)

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.