Habari za Punde

MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO AONGOZA MAZOEZI KUITIKIA AGIZO LA MAKAMU WA RAIS

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Saidi Mecki Sadiki akiwa na viongozi wengine wa kiserikali wakiowaongoza watumishi wa kada mbalimbali ,watumishi wa umma,wanafunzi wa shule za msingi na sekondari katika uzinduzi wa kampeni ya kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza kwa njia ya mazoezi kimkoa.
Washiriki wa zoezi hilo wakipita maeneo mbalimbali ya mji Moshi kwa kutembea na kukimbia kidogo kidogo. KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
Mazoezi ya awali ya kukimbia na kutembea yaliyoanzia ofsi ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,yalihitimishwa kwa mazoezi ya viungo katika uwanja wa Chuo Kikuu chuo kikuu cha Ushirika mjini Moshi. 
Askari kutoka vikosi mbalimbali vya Jeshi la Polisi pia walishiriki vyema mazoezi hayo. 
Katibu Tawala mkoa wa Kilimanjaro,Mhandisi Aisha Amour alikuwa ni miongoni mwa washiriki katika mazoezi hayo. 
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira mjini Moshi,Joyce Msiru pia alishiriki katika mazoezi hayo.
Wanafunzi kutoka shue mbalimbali za sekondari na msingi pia walikuwepo. 
Jeshi la Magereza pia liliwakilishwa vyema na baadhi ya askari wake. Picha ba Dixon Busagaga, Kanda ya Kaskazini. 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.