Habari za Punde

MWENYEKITI WA SERIKALI YA MTAA MBEZI KATI AANZA ZOEZI LA KUWATIMUA MACHINGA TANGI BOVU

 Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mbezi Kati, Mc Double A, akiwakoromea wafanyabiashara wa matunda na mbogamboga katika Kituo cha daldala cha Tangi Bovu leo jioni wakati akiwakemea kuwataka kuondoa bishara zao pembezoni mwa Barabara na kituo hicho ambacho kwa sasa kimekua ni kero kwa wapita njia na abiria kutokana na wafanya biashara hao kupanga biashara zao bila kufuata utaratibu.

Imeelezwa kuwa wafanyabiashara hao waliruhusiwa kupanga biashara zao pembezoni mwa Barabara ya Dharura 'Service Road' lakini wao wakajiongeza kwa kuvamia hadi pembezoni mwa barabara kubwa na vituo vya daladala.
'Aroo wewe usiendelee kupanga hapa hebu inuka uniangalie na unisikilize''
 Huyu mwenye viatu yuko wapi???????
 Aroo naongea na nyie mnanichunia eeeh mnajifanya hamnisikii eeeh???

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.