Habari za Punde

PAUL MAKONDA ATAJA MAJINA MAPYA 65 WAMO, MBOWE, AZAN,GWAJIMA NA MANJI

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo amewataja watuhumiwa wengine 65 wa Dawa za Kulevya akiwemo Freeman Mbowe, Mchungaji Gwajima, Yusuf Manji na Idd Azzan. 
Aidha Mkuu wa Mkoa amewataka Vigogo hao kufika kituo cha Polisi siku ya Ijumaa kwa ajili ya kuhojiwa.

Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam,Paul Makonda amewataja watuhumiwa 65 wa Dawa za Kulevya,katika majia hayo ametajwa Freeman Mbowe,Mchungaji Gwajima,Yusuf Manji,Idd Azzan.
Akizungumza na waandishi wa habari Ofisi kwake mapema leo jijini Dar,RC Makonda ameingia katika awamu ya pili ya kutaja majina hayo na kuyaweka hadharani,huku akieleza kuwa watuhumiwa hao watatakiwa kufika kituo cha polisi kati siku ya Ijumaa,saa tano asubuhi kwa mahojiano zaidi.

Katika hatua nyingine RC Makonda amekiri kukamatwa kwa Mmiliki wa kituo cha Radio ya EFM,ajulikanae kwa jina la Francis Ciza,almaarufu kwa jina la Dj Majay."tulipokuwa tukifanya opereseheni ya kuwakamata Wahusika weote wa Dawa za kulevya juzi usiku nae akakamatwa kw mahojiano zaidi;"alisema Makonda.
Makonda amejibu habari za kukamatwa kwa Dj Majay mara baada ya kuulizwa swali na mmoja wa waandishi wa habari,kufuatia tetesi nyingi zilizokuwa zikisambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii.
Soma zaidi majina ya watuhumiwa wa sakala hilo la Dawa za kulevya.


No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.