Habari za Punde

RC IRINGA AINGIA DARASANI KUFUNDISHA , AAGIZA WILAYA YA MUFINDI KUINGIA 10 BORA UFAULU KITAIFA

Mkuu wa mkoa wa Iringa Mwalimu Amina Masenza akiendelea kufundisha wanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari sadani 
Mkuu wa mkoa wa Iringa mwalimu Amina Masenza akifundi somo la Uraia kwa wanafunzi wa kidato cha tano shule ya sekondari Sadani wilaya ya Mufindi leo baada ya kufanya ziara shuleni hapo
Mkuu wa mkoa wa Iringa mwalimu Amina Masenza akipokelewa shule ya sekondari Sadani 
Mkuu wa wilaya ya Mufindi Wiliam Jamhuri akimkaribisha mkuu wa mkoa wa Iringa 
Watalam wa mkoa wa Iringa. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Walimu na viongozi wa wilaya ya Mufindi.
Watumishi wakimsikiliza mkuu wa mkoa.
Mkuu wa shule ya sekondari Sadani Mufindi Yusuph Mwagala.
Mkuu wa shule ya sekondari Sadani Mufindi Yusuph Mwagala akipongezwa na mkuu wa mkoa wa Iringa Mwalimu Amina Masenza,
Mkuu wa mkoa wa Iringa mwalimu Amina Masenza na mkuu wa wilaya ya Mufindi Wiliam Jamhuri wakifungua daharia ya wasichana shule ya sekondari Sadani 
Rc akikagua daharia hiyo 
Bwalo la chakula Sadani Sekondari ambalo linahitaji wadau kuchangia ili kukamilika 
Rc Mwalimu Masenza akitoka kukagua bwalo hilo 
Mwanafunzi wa kidato cha sitta Sadani sekondari Sagendo Fadhili akijibu maswali ya mkuu wa mkoa wa Iringa Mwalimu Amina Masenza 
Mkuu wa mkoa wa Iringa mwalimu Amina Masenza akiwa na mkuu wa shule ya Sadani katikati na mkuu wa wilaya ya Mufindi Bw Wiliam Jamhuri kushoto
Walimu wa Sadani Sekondari wakifurahia ziara ya mkuu wa mkoa shuleni hapo na kuomba kusaidiwa kusogezewa umeme wa Rea shuleni hapo 
Mwalimu Masenza mkuu wa mkoa wa Iringa akiteta na walimu wenzake wa shule ya sekondari Sadani Mufindi 
Mkuu wa mkoa wa Iringa Mwalimu Amina Masenza (wa nne kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na walimu wa shule ya sekondari Sadani 
MKUU wa mkoa wa Iringa Amina Masenza amelazimika kuingia darasani kufundisha kama njia ya kuwataka walimu kuwajibika kufundisha huku akiuagiza uongozi wa wilaya ya Mufindi kuhakikisha wanaweka mikakati itakayoiwezesha shule ya sekondari ya Sadani kuingia katika nafasi ya 10 bora katika mitihani ya kitaifa mwakani 2018.

Huku akichangia kiasi cha Tsh milioni 1 kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wanafunzi shuleni hapo kama sehemu ya maandalizi ya shule hiyo kujiandaa kuwa shulebora kitaifa.

Mkuu huyo wa mkoa ametoa agizo hilo leo wakati wa ziara yake ya ukaguzi na ufunguzi wa bweni la wanafunzi wa kike katika shule hiyo,kuwa kutokana na mkoa wa Iringa kufanya vema katika mitihani ya Kitaifa ya kidato cha nne kwa kuwa mkoa wa pili kitaifa ila bado wilaya ya Mufindi inapaswa kuhakikisha shule hiyo kuwa kati ya shule 10 bora kitaifa .
Alisema kuwa moja katika ya maagizo ambayo anataka mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mufindi kufanya ni kuandaa mkataba maalum, kati ya waslimu wa shule hiyo ya mkurugenzi mkataba ambao atausaini kwa ajili ya ofisi yake na mkuu wa wilaya ya Mufindi kuingia mkataba iwapo watashindwa kuingia katika shule 10 bora basi watamtafuta aliyekwamisha mkataba illi achukuliwe hatua.
“ Mkataba hii itakuwa kwa walimu wote wa mkoa wa Iringa ili kupima uwezo wa walimu katika kutimiza wajibu waokatika utendaji kazi ili kama mwalimu asiyewajibika basi kukaa pembeni ili kupisha mwalimu ambae anafanya kazi kwa ari ya kujituma zaidi”
Hata hivyo aliwataka walimu kufanya kazi kwa kutimiza wajibu wao badala ya kufanya kazi kwa mazoea kwa kukimbilia kudai haki zao badala ya kufuata taratibu.
Alisema wapo baadhi ya walimu wanalalamika kudai haki zao ila wamekuwa wakiendea kutibiwa nje ya mkoa bila hata ya kufuata taratibu za kuandika barua na kuwataka kuzingatia taratibu za kazi kwa kutunza kumbukumbu mbali mbali katika mafaili yao.
Kuhusu ujenzi bweni na umaliziaji wa bwalo la chakula shuleni hapo aliagiza mkuu wa wilaya kuitisha kikao na wafanyabiashara ili kusaidia ujenzi huo na shughuli za kimaendeleo shuleni hapo.
Pia alipongeza jitihada kubwa zinazofanywa na uongozi wa shule hiyo chini ya mkuu wake Yusuph Mwagala kutokana na kuendelea kufanya shule hiyo kuwa mbeli kielimu pamoja na maendeleo mengine.
Awali mkuu wa shule hiyo Bw Mwagala alisema kuwa shule hiyo imeendelea kufanya vema katika nafasi ya kimkoa na kitaifa ambapo mwaka 2015 katika matokeo ya kidato cha nne ilishika nafasi ya 64 kati ya shule 131 kimkoa na kiwilaya ilishika nafasi ya 26 kati ya shule 54 wakati kwa mwaka huu imeshika nafasiya 25 kati ya shule 152 kimkoa na nafasi ya 8 kati ya 42 kiwilaya 

Pia alisema mbali ya mafanikio katika elimu bado shule hiyo inakabilia na changamoto mbali mbali kamaupungufu wa mabweni ya wanafunzi wa kidato cha tano na sita upungufu ambao unatokana na ongezeko kubwa la udahiri wa wanafunzi wa kidato cha tano kulingana na miundo mbinu iliyopo kabla ya kuanzisha kidato cha tano na sita ,upungufu na uchakavu wa vyumba vya madarasa,ukosefu wa umeme ,ukosefu wa bwalo la chakula, upungufu wa walimu 8 wa masomo ya sayansi ,walimu watatu wa somo la biolojia, walimu wawili wa masomo ya fizikia ,walimu watatu wa kemia na hesabu mwalimu mmoja ,ukosefu wa maabara ya biolojia.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.