Habari za Punde

SIMBA WAIPOKA YANGA 'BANDO LA WIKI ' WAREJEA KILELENI WAKIICHAPA TZ PRISONS 3-0
SIMBA leo imerejea tena kileleni mwa Ligi Kuu Bara baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.Simba sasa wanafikisha jumla ya pointi 51 na kuwaengua kileleni watanani zao wa Jadi Yanga waliokuwa wakiongoza Ligi hiyo kwa tofauti ya pointi 1 wakiwa na Pointi 49.

Yanga wao wameondoka leo asubuhi kuelekea Comoro katika mechi ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika ambapo wakirejea Feb 18 watakuwa na mchezo wa marudiano na Wacomoro hao na baada ya hapo wataanza mawindo ya mchezo wao wa Ligi dhidi ya Mtani wao Simba unaotarajia kupigwa Feb 25.

Katika mchezo huo, Simba waliandika bao la kwanza katika dakika ya 18 lililofungwa na Juma Luizio baada ya kupigwa kona ya `nje’ kabla ya mpira kumkuta mfungaji aliyeujaza wavuni.
Dakika 10 baadae Simba waliandika bao la pili kupitia kwa Ibrahim Ajibu akiunganisha krosi ya Loudit Mavugo.
Simba waliandika bao la tatu kupitia kwa Loudit Mavugo kwa kichwa akiunganisha krosi ya Ajibu.

Simba: Daniel Agyei,Method Mwanjale/Mwinyi Kazimoto, Javier Bukungu, Mohamef Hussein, Novalty Lufunga, Said Ndemla, James Kotei, Mzamiru Yassin, Ibrahim Ajibu/Pastor Athanas, Laudit Mavugo na Juma Luizio/Shiza Kichuya.
Prisons: Laurian Mpalile, Aron kalambo, Salum Kimenya, James Mwasote, Nurdin Chona, Jumanne Elifadhili, Lambart Sabiyanka, Kazungu Nchinjayi/Kassim Hamis, Victor Hangaya, Mohamed Samata na Benjamin Asukile/Meshaki Selemani.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.