Habari za Punde

TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) KWA KUSHIRIKIANA HOSPITALI YA BLK YA NCHINI INDIA WATOA HUDUMA YA MATIBABU YA MOYO BILA KUPASUA KIFUA KWA WAGONJWA 16

  Madaktari Bingwa wa Moyo kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge (kushoto) na Subhash Chandra (kulia) kutoka Hospitali ya  BLK ya nchini India wakimwekea mgonjwa kifaa kitakachosaidia moyo kupata umeme kwa jina la kitaalam Pacemaker . JKCI kwa kushirikiana na BLK hospital kwa kutumia mtambo wa Cath Lab wamewafanyia wagonjwa 16 huduma  mbalimbali za matibabu ya moyo ya  bila kufungua kifua (Catheterization). 
Daktari bingwa wa  Moyo wa Taasisi ya Moyo  Jakaya Kikwete (JKCI) Peter Kisenge akimuhudumia Monica Mahenge ambaye amelazwa katika Taasisi hiyo baada ya kufanyiwa matibabu ya moyo kupitia mishipa ya damu  bila kufungua kifua (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cath lab . Monica ni mmoja kati ya wagonjwa 16 ambao JKCI kwa kushirikiana na wataalamu kutoka Hospitali ya BLK ya nchini India walitoa huduma za matibabu ya kuzibua milango ya moyo (Valve), balloon mitral valve  procedure (Valvuloplasty), kuzibua mishipa ya damu ya moyo,  kufunga kifaa kitakachosaidia moyo kupata umeme (Pacemaker) na kuangalia utendaji kazi wa Moyo.
 Madaktari bingwa wa  Moyo, Wauguzi, Technologists, wataalam wa dawa za usingizi  wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kumpatia mgonjwa huduma za matibabu ya kuzibua milango ya moyo (Valve) bila kufungua kifua (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cath lab.
Kazi ya kutoa huduma ya matibabu ya Moyo kwa  mgonjwa  kupitia mishipa ya damu  bila kufungua kifua (Catheterization) kwa kutumia mtambo wa Cath lab ikiendelea. Picha na Anna Nkinda – JKCI

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.