Habari za Punde

TFF YAITAKIA KILA LA KHERI TIMU YA YANGA MCHEZO WAKE WA KIMATAIFA KESHO

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linachukua nafasi hii kuitakia kila la kheri timu ya Young Africans katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo hatua ya awali imeanza wikiendi hii.
Wakati Young Africans inacheza, kesho Februari 12, mwaka huu, Azam itasubiri mshindi kati ya Mbabane Swallons ya Swaziland na Opara United ya Botswana katika michuano ya Kombe la Shirikisho (CAF).
Timu ya Young Africans ambayo ni mabingwa wa Tanzania inayoiwakilisha nchi katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kesho Jumapili Februari 12, 2017 inacheza na Ngaye De Mbe ya Nchini Comoro.
“Tunaitakia Wawakilishi wa nchi Young Africans ya Tanzania kila la kheri,” amesema Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.