Habari za Punde

TFF YATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI VIFO VYA MASHABIKI ANGOLA

Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF), limepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za vifo vya mashabiki 17 na wengine kujeruhiwa katika tukio la watu kukimbia uwanjani kwa tishio la mabomu wakati wa mchezo wa timu mbili zenye ushindani.
Maelfu ya mashabiki, wakiwamo watoto wadogo walianza kukimbia na wengine kukanyagana hali iliyosababisha vifo uwanjani.
Rais Jamal Malinzi wa TFF, ameelezea kushtushwa na taarifa hizo za vifo hivyo vilivyoripotiwa kutokea Ijumaa Februari 10, 2017 kwenye Uwanja wa Angola ulioko mjini Uige, Kaskazini mwa nchi hiyo. 
Kwa masikitiko makubwa, Rais wa TFF Malinzi ametuma salamu zangu za rambirambi kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Angola (AFF); familia za ndugu waliopoteza wapendwa wao katika maisha, watu wa nchi hiyo, kutokana na vifo hivyo.
Rais Malinzi amesema kwa nguvu za Mungu anawaombea heri ya kupona majeruhi na kwamba Tanzania inasali kuwaombea watu wa Angola wakati huu mguu.
Mwenyezi Mungu azipokee roho za marehemu mahali pema peponi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.