Habari za Punde

UJENZI WA JENGO JIPYA LA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE (TERMINAL 3) WAENDELEA LEO MARA BAADA YA RAIS KUTOA AGIZO JANA.

Shughuli za Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal 3) ukiendelea mbele ya Jengo jipya la Abiria kama inavyoonekana pichani kufatia ziara ya kushtukiza ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyofanya hapo jana na kutoa Maagizo kwa Mkandarasi wa Uwanja huo kuanza kazi mara moja kuanzia leo.
Kazi ya Umwagiliaji ikiendelea katika sehemu ya mbele ya ya Jengo jipya la Abiria kama inavyoonekana pichani.
Mmoja wa Mafundi akiendelea kazi ndani ya jengo hilo la Abiria uwanjani hapo.
Mafundi Umeme wakiendelea na kazi ndani ya jengo hilo la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal 3).
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa Moja ya nguzo katika jengo hilo la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal 3).
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa sehemu ya chini ya maegesho ya ndege kama inavyoonekana.
Mafundi wakiendelea na ujenzi sehemu ya juu ya jengo hilo la Abiria kama inavyoonekana.
Sehemu ya mbele ya jengo hilo la Abiria kama linavyoonekana. PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.