Habari za Punde

UZINDUZI WA JUKWAA LA BIASHARA MKOANI SIMIYU

Na Mroki Mroki, Simiyu 
Ni ile siku iliyosubiriwa ya kuumulika kibiashara mkoa wa Simiyu ulioanzishwa mwaka 2012, ambao umejipambanua kuwa ‘mkoa darasa’, mintarafu suala zima la ujenzi wa viwanda nchini.
Mwezi uliopita, Rais John Magufuli alipotembelea mkoa huu, alipongeza juhudi zinazochukuliwa na mkoa huu chini ya mkuu wake, Anthony Mtaka, katika kujenga uchumi wa viwanda na hivyo kuelekea kuifanya ndoto yake ya Tanzania ya viwanda kutimia.
Kupitia Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) inayochapisha magazeti ya Daily News na HabariLeo pamoja na mitandao mbalimbali ya kijamii, imeshirikiana na Mkoa wa Simiyu kuandaa Jukwaa la Biashara Simiyu likiwa na lengo la kuibua fursa za uchumi za mkoa huu darasa ambazo zitadadavuliwa na kuchambuliwa hii leo, na hivyo kuwasaidia wawekezaji wa ndani na nje kujua ‘kunani’ Simiyu.
Mkuu wa Mkao wa Simiyu, Anthony Mtaka (kulia) akifurahia jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Elisante Ole Gabriel katika Jukwaa hilo la Biashara Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka akizungumza wakati wa ufunguzi wa Jukwaa la Biashara Mkoa wa Simiyu ambapo alilisitiza kuwa Simiyu itajengwa na wana Simiyu wenyewe na si kutegemea watu kutoka nje. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof Elisante Ole Gabriel akitoa mada katika Jukwaa la Biashara Simiyu.Prof aliwataka wafanyabiashara kutambia biashara wanayoifanya maana wateja hawanunui biadhaa zao bali hununua thamani ya kitu kinachouzwa. 
Mbunge wa Jimbo la Itim,ila Mkoani Simiyu na Mwenyekiti wa Wafanyabiashra Simiyu, Njalu Daudi Silanga akizungumza machache kuhusiana na Jukwaa hilo la Biashara Simiyu. 
Mbunge wa Busega, Dk Raphael Chegeni akizungumza na kupongeza jitihada hizo za kuutangaza mkoa wa Simiyu na fursa zake zilizopo katika kukuza uchumi na maendeleo ya wanasimiyu.
Mbunge wa Busega, Dk Raphael Chegeni akisoma gazeti la Habari leo.
Meza Kuu.
Washiriki wa Jukwaa hilo la Biashara Simiyu.
Baadhi ya wafanyabiashra wa Mkoani Simiyu wakiwa katika Jukwaa hilo.
Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magzeti ya Serikali (TSN) wachapishaji wa magfazeti ya Daily News, Habarileo na Spotileo ambao pia ni wamiliki wa Kiwanda cha Uchapaji cha Standard Printer, DK Jim Yonazi akizungumza na kueleza kwanini wameanza na Simiyu katika kuvumbua fursa. 
Meza Kuu ikimsikiliza Mhariri Mtendaji wa TSN, Dk Jim Yonazi.
Washiriki

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.