Habari za Punde

WADAU WA SEKTA YA FILAMU WAKUTANA NA VIONGOZI WA WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO KUJADILI SERA YA FILAMU

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (kushoto) akizungumza na wadau wa sekta ya filamu (hawapo pichani) wakati wa kikao cha wadau kuzungumzia sera ya filamu leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura na Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi. Nuru Millao.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akifafanua jambo wakati wa kikao cha wadau wa sekta ya filamu kuzungumzia sera ya filamu leo Jijini Dar es Salaam.
Mtayarishaji na msambazaji wa filamu nchini Bibi. Rose Urio akichangia mada wakati wa kikao cha wadau wa sekta ya filamu kuzungumzia sera ya filamu leo Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Bw. Godfrey Mngereza akitolea ufafanuzi maoni yaliyotolewa wakati wa kikao cha wadau wa sekta ya filamu kuzungumzia sera ya filamu leo Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau wa sekta ya filamu wakisikiliza hoja zilizokua zikiendelea kutolewa wakati wa kikao cha wadau kuzungumzia sera ya filamu leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (wanne kulia) katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa sekta ya filamu walioshiriki katika kikao cha wadau kuzungumzia sera ya filamu leo Jijini Dar es Salaam. Watatu kulia ni Naibu Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura, watano kulia ni Katibu Mkuu Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel na wapili kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi. Nuru Millao. Picha na: Genofeva Matemu WHUSM.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.