Habari za Punde

WASANII MBALIMBALI WEMA NA WENZAKE WALIVYORIPOTI KITUOCHA POLISI KATI JANA KUHOJIWA

Msanii wa bongo movie, Wema Sepetu, (mwenye mkopa), akisindikizwa kuingia kituo kikuu cha polisi cha jijini Dar es Salaam, Februari 3, 2017. Wema na wasanii wenzake wengine wawili na mtangazaji mmoja wa Televisheni, waliripoti kituoni hapo kufuatia agizo la mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, la kuwataka wafanye hivyo ili wazungumzie tuhuma zinazohusiana na uuzaji na matumizi ya madawa ya kulevya. 

Katika mkutano wa pamoja na Waandishi wa habari uliofanyika kituo kikuu cha polisi Dar es Salaam, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, ametangaza orodha mpya ya watuhumiwa wa kutumia na kuuza madawa ya kulevya akiwemo msanii wa Bongo Fleva, Vanes Mdee. 

Watu kadhaa jijini Dar es Salaam, wakiwemo polisi, wametajwa na Mkuu huyo wa mkoa, akiwatuhumu kujihusisha kwa namna moja au nyingine katika biashara hiyo haramu ya madawa ya kulevya. 

Mkuu wa Mkoa Makonda, alitoa orodha ndefu ya watu waliotakiwa kuripoti leo kituoni hapo Alhamisi ya Februari 2, 2017. Hata hivyo Makonda ameagiza watuhumiwa ambao walitakiwa kuripoti leo na kukaidi agizo lake, wasakwe na kutiwa mbaroni. 

Miongoni mwa wanaotafutwa na msanii Chidi Benz. Naye Kamanda wa polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, Simon Siro, alisema, Kanda yake imeunda kikosi kazi cha kutekeleza ahizo la mkuu wa mkoa ambapo kitahusisha vyombo vyote vya ulinzi na usalama. 

Kamanda Siro pia alikiri kuwashikilia kwa mahojiano wasanii Wema Sepetu na wenzake pamoja na askari polisi saba kati ya tisa wanaotuhumiwa.
TID akiwasili kituo kikuu cha kati cha polisi jijini Dar es Salaam, Februari 3, 2017
Mtangazaji wa Clouds TV, ajulikanaye kama mzee wa Kitaa, akiwasili kituo kikuu cha polisi Dar es Salaam, kuitikia wito wa Mkuu wa Mkoa huo Paul Makonda.
Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Siro, akiwa anafuatwa na waandishi wa habari alipowasili kituoni hapo
Waandishi an wananchi wakiwa wamepiga kambi nje ya geti la kingilia kituo kikuu cha polisi Kati jijini Dar es Salaam
Waandishi an wananchi wakiwa wamepiga kambi nje ya geti la kingilia kituo kikuu cha polisi Kati jijini Dar es Salaam
Polisi akitoa maelekezo
Kamanda Siro, (kushoto), akiwasili kituoni hapo

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.