Habari za Punde

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AZIAGIZA HALMASHAURI ZOTE NCHINI KUTENGA MAENEO YA KUFANYIA MAZOEZI

Na. Lilian Lundo - MAELEZO - Dodoma.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameziagiza Halmashauri, Manispaa na Majiji yote nchini kutenga maeneo kwa ajili ya watu kufanya mazoezi na kupumzika.

Kassim Majaliwa ametoa agizo hilo leo, Mjini Dodoma katika uzinduzi wa Kitaifa wa mazoezi ya viungo kwa wananchi wote yaliyofanyika katika viwanja vya Jamhuri.
"Ni muhimu kufanya mazoezi kila siku, mazoezi yanasaidia kuchangamsha mwili, kufahamiana, kujenga urafiki pamoja na kuwa na afya bora," alifafanua Kassim Majaliwa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (aliyevaa traksuti nyeusi) akiwa ameongozana na Viongozi mbalimbali kuelekea Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma kwenye Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa Wananchi wote yaliyofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo 11/02/2017. 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (aliyevaa traksuti nyeupe) akiwa ameongozana na Viongozi mbalimbali kuelekea Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma kwenye Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa Wananchi wote yaliyofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo 11/02/2017. 
Kikosi cha Bendi ya Matarumbeta ycha Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wakiongoza matembezo kuelekea Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma kwenye Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa Wananchi wote yaliyofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo 11/02/2017. 
Umati wa watu pamoja na Jeshi la Wananchi Tanzania wakiwa katika matembezi kuelekea Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma kwenye Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa Wananchi wote yaliyofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo 11/02/2017. 
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (wa pili kulia), Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (wa pili kushoto) pamoja na Viongozi wengine wakifanya mazoezi kuelekea Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma kwenye Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa Wananchi wote yaliyofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo 11/02/2017. 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (aliyevaa traksuti nyeupe) akiongoza mazoezi ya viungo wakati wa Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa Wananchi wote yaliyofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo 11/02/2017.  KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akiwahutubia baadhi ya Viongozi wa Serikali pamoja na wananchi (hawapo pichani) waliohudhuria Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa Wananchi wote yaliyofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo 11/02/2017. 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye akitoa neno la shukrani mbele ya Viongozi wa Serikali pamoja na wananchi waliohudhuria Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa Wananchi wote yaliyofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo 11/02/2017. 
Waziri Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu akiongelea kuhusu umuhimu wa mazoezi katika kulinda afya, mbele ya Viongozi wa Serikali pamoja na wananchi waliohudhuria Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa Wananchi wote yaliyofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo 11/02/2017. 
Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu(Vijana, Kazi na Ajira), Mhe. Anthony Mavunde, akiongea jambo akiwa kama Kiongozi mwakilishi wa Mkoa wa Dodoma, mbele ya Viongozi wa Serikali pamoja na wananchi waliohudhuria Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa Wananchi wote yaliyofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo 11/02/2017. 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (kulia) akiongea na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo leo mara baada ya kumalizika kwa Uzinduzi wa Kitaifa wa Mazoezi ya Viungo kwa Wananchi wote yaliyofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma leo 11/02/2017.  
PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-WHUSM
******************************************************
Aidha, Majaliwa amesema kwamba muitikio wa ufanyaji mazoezi ya viungo ni mkubwa, watu wengi wamejiunga na vikundi mbalimbali vya kufanya mazoezi ya viungo.
Hivyo basi amezitaka Halmashauri, Manispaa na Majiji yote nchini kutenga maeneo kwa ajili ya watu kufanya mazoezi na kumpizika.
Aidha, amesema kuwa, watu wasilazimishwe kufanya mazoezi bali iwe ni hiari ya mtu na kusiwe na gharama kwa ajili ya mtu kufanya mazoezi.
Amewataka Maafisa Utamaduni na Michezo kuhamasisha mazoezi ya viungo katika maeneo yao pamoja na kuanzisha vikundi vya mazoezi ya viungo ambapo watakuwa wanakutana na kufanya mazoezi kwa muda ambao watajipangia.
Kwa upande wake, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amemshukuru Makamu wa Rais Samia Suluhu kwa kuhamasisha mazoezi ya viungo na kuitangaza rasmi Jumamosi ya pili ya mwezi kuwa ni siku ya mazoezi ya viungo Kitaifa.
Aliendelea kwa kusema kuwa mazoezi ya viungo yanamuepusha mtu na kupata magonjwa yasiyoambukiza kama vile magonjwa ya moyo, kisukari na saratani.
Nae, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye amesema kuwa mazoezi ya viungo yanaratibiwa na Wizara ya Habari, Wizara ya Afya na TAMISEMI. Hivyo kwa pamoja watahamasisha uanzishwaji wa vikundi vya mazoezi ya viungo katika Halmashauri zote nchini kwa kuanza na watumishi wa Umma.
Aidha, Nape amewataka viongozi wanapokuwa mikoani katika siku ya mazoezi ya viungo kuhamasisha mazoezi ya viungo kwa kufanya mazoezi na wananchi.
Uzinduzi wa Kitaifa wa mazoezi ya viungo ulianza kwa matembezi yaliongozwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu kuanzia viwanja vya Bunge na baadae alimkabidhi Waziri Mkuu kuanzia Nyerere Square mpaka Uwanja wa Jamhuri. Uzinduzi huo umehusisha viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri, Wabunge, Viongozi wa Mkoa wa Dodoma na Wananchi wa Mkoa huo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.