Habari za Punde

WAZIRI NAPE AFANYA MSAKO KARIAKOO LEO KUKAMATA WANAODURUFU KAZI ZA WASANII

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akiingia katika moja ya stoo za Duka mojawapo linalouza na kudurufu kazi za wasanii mbalimbali nchini.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuhitimisha ziara yake hiyo katika eneo la Kariakoo, Jijini Dar es salaam leo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (katikati) akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa Idara ya Habari - MAELEZO, Dkt. Hassan Abbas (kushoto) pamoja na maafisa wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), wakia katika oparesheni maalum ya kushtukiza la kukamata wafanyabiashara wanaodurufu kazi mbalimbali za sanaa nchini, katika eneo la Karikoo jijini Dar es salaam leo. KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (kushoto) akiongoza msafara huo wa kufanya oparesheni maalum ya kushtukiza la kukamata wafanyabiashara wanaodurufu kazi mbalimbali za sanaa nchini, katika eneo la Karikoo jijini Dar es salaam leo. Picha na Iman Nsamila.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akiangalia baadhi ya DVD feki zilizokuwepo katika moja ya maduka ya Kariakoo, Jijini Dar es salaam leo.
Baadhi ya Maafisa wa TRA wakichukua maelezo ya mmoja wa wafanyabiashara wa Duka hilo, huku Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akiendelea kizitazama zingine.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akielekeza jambo wakati alipotembelea moja ya Duka linalouza kazi feki za sanaa mbalimbali.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akimsikiliza mmoja wa wafanya biashara hao.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.