Habari za Punde

WAZIRI NAPE: UTAMADUNI WA MTANZANIA NI SEHEMU YA KIVUTIO CHA UTALII

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akizungumza wakati wa kilele cha Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni baina ya Shiraz na Tanzania leo jijini Dar es Salaam.  Maonyesho hayo yalikuwa na kauli mbiu ya “Ushirikiano wa Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya kukuza na kuendeleza Lugha,Sanaa na Filamu,Mila na desturi zake”.
 Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Makumbusho ya Taifa Profesa Audax Mabulla akizungumza wakati wa kilele cha Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni baina ya Shiraz na Tanzania leo jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo yalikuwa na kauli mbiu ya “Ushirikiano wa Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya kukuza na kuendeleza Lugha,Sanaa na Filamu,Mila na desturi zake”.
 Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Iran nchini Tanzania Mossa Farharng (wa pili kutoka kushoto) akifuatilia hotuba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye (hayupo pichani) wakati wa kilele cha Wiki ya Utamaduni wa Shiraz iliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa Profesa Audax Mabulla, Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Iran Ali Bagheri na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akicheza Bao na Mwenyekiti wa Shirikisho la Michezo ya Jadi Tanzania Bw. Mohamed Kazingumbe (kulia) wakati wa kilele cha Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni baina ya Shiraz na Tanzania leo jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo yalikuwa na kauli mbiu ya “Ushirikiano wa Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya kukuza na kuendeleza Lugha,Sanaa na Filamu,Mila na desturi zake”.
Baadhi ya Wasanii kutoka Iran wakitumbuiza muziki wa Ala wakati wa kilele cha Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni baina ya Shiraz na Tanzania leo jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo yalikuwa na kauli mbiu ya “Ushirikiano wa Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya kukuza na kuendeleza Lugha,Sanaa na Filamu,Mila na desturi zake”.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akiangalia moja ya vitabu vyenye maneno ya Kishiraz wakati wa kilele cha Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni baina ya Shiraz na Tanzania leo jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo yalikuwa na kauli mbiu ya “Ushirikiano wa Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya kukuza na kuendeleza Lugha,Sanaa na Filamu,Mila na desturi zake”. Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Bibi. Lilian Beleko, Balozi wa Iran nchini Mossa Farharng na Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Iran Ali Bagheri.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akisikiliza maelezo kuhusu michoro ya Kiutamaduni ya Iran wakati wa kilele cha Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni baina ya Shiraz na Tanzania leo jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo yalikuwa na kauli mbiu ya “Ushirikiano wa Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya kukuza na kuendeleza Lugha,Sanaa na Filamu,Mila na desturi zake”.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akifurahia jambo mara baada ya kupata maelezo ya namna ya kufanya marekebisho ya Vitabu kutoka kwa Ali Navidogooe Shiraz wakati wa kilele cha Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni baina ya Shiraz na Tanzania leo jijini Dar es Salaam. Maonyesho hayo yalikuwa na kauli mbiu ya “Ushirikiano wa Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya kukuza na kuendeleza Lugha,Sanaa na Filamu,Mila na desturi zake”.
  Wasanii wa Mashairi Bw. Issa Amiri Kilimo aka. Kijoka Kidogo na Mwajuma Seleman Yombe wakiimba shairi kwa njia ya majibizano ikiwa ni kujibu shairi la Siri la mtunzi Haji Myaka bin Haji la mwaka 1405 le jijini Dar es Salaam wakati wa kilele cha Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni baina ya Shiraz na Tanzania.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akipiga Gitaa  lililotengenezwa na Msaanii wa Uchoraji na Uchongaji Bw. Washington Steven Masanja (kushoto) wakati wa kilele cha Maonyesho ya Wiki ya Utamaduni baina ya Shiraz na Tanzania leo jijini Dar es Salaam.Maonyesho hayo yalikuwa na kauli mbiu ya “Ushirikiano wa Kiutamaduni ni nguzo muhimu ya kukuza na kuendeleza Lugha,Sanaa na Filamu,Mila na desturi zake”. Kushoto kwa Waziri ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo.
 Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Iran nchini Tanzania Mossa Farharng akimkabidhi zawadi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye  wakati wa kilele cha Wiki ya Utamaduni wa Shiraz iliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam leo. 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akifurahia jambo na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Iran nchini Tanzania Mossa Farharng wakati wa kilele cha Wiki ya Utamaduni wa Shiraz iliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam leo. 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa Iran nchini Tanzania Mossa Farharng na baadhi ya viongozi kutoka taasisi za Serikali na ubalozi wa Iran wakati wa kilele cha Wiki ya Utamaduni wa Shiraz iliyofanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam leo. Picha na: Frank Shija – MAELEZO.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.