Habari za Punde

WLAC WAANZISHA MDAHALO KWA WANAFUNZI WA SHULE ZA SEKONDARI NA VYUO KUHUSU UKATILI WA KIJINSIA

 Mwezeshaji, Shaban Rashid, akiendesha mdahalo kwa wanafunzi wa Chuo cha Data Star Training College, wakati wakiwa katika mjadala huo kuhusu Ukatili wa Kijinsia ni Chanzo cha kushuka kwa Maendeleo ya Elimu kwa Watoto wa Kike. Mjadala huo uliofanyika leo chuoni hapo unatarajia pia kufanyika katika Shule za Sekondari, Mbezi Hi School, Jangwani Sec, Kibasila Sec, Yusuph Makamba Sec, Mama Salma Kikwete Sec, Ebenito College, Royal College na Chuo cha Usafirishaji NIT.
Mafunzo hayo yameandaliwa na Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake na Watoto WLAC kupitia mradi wa Kampeni ya 'TUNAWEZA' unaodhaminiwa na Oxfarm.
 Mwezeshaji, Shaban Rashid, akiendesha mdahalo kwa wanafunzi wa Chuo cha Data Star Training College.
 Sehemu ya wanafunzi wa Chuo hicho wakiwa katika mdahalo huo.
 Mdahalo ukiendelea....
 Mwanafunzi wa Chuo hicho, Naima Said,akichangia mada wakati wa mdahalo huo leo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.