Habari za Punde

YANGA YAANZA VYEMA MICHUANO YA LIGI YA MABINGWA AFRIKA KWA KUWABANJUA NGAYA MABAO 5-1

Na Ripota Wetu, Comoro
TIMU ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, leo wameanza vyema michuano ya Klabu Bingwa Afrika kwa kuwabanjua wenyeji wao Ngaya Club de Mde kwa jumla ya mabao 5-1 katika mchezo uliopigwa leo mjini Moroni, Comoro.
Baada ya ushindi huo Yanga wanatarajia kurudiana na wapinzani wao hao Jumamosi ya wiki ijayo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ambapo inaonesha kuwa tayari wamejinyooshea njia ya kusonga mbele.
Bao la kwanza lilifungwa na Kiungo Mzambia, Justin Zulu katika dakika ya 43,bao la pili likifungwa na Simon Msuva katika dakika ya 45.
Bao la tatu lilifungwa na Obrey Chirwa katika dakika ya 59, bao la Nne lilifungwa na Amissi Tambwe, katika dakika ya 65 na la tano likifungwa na Thabani Kamusoko katika dakika ya 73.
Ngaya walijipatia bao lao la kufutia machozi katika dakika ya 66 likifungwa na Said Anfane Bourah Mohammed aliyetokea benchi kipindi cha pili.

KIKOSI CGA NGAYA: Said Mmadi, Said Hachim, Said Tothir, Adhepeau Denis Hubert, Ali Ahmada, Youssouf Ibrahim Moidjie, Zamir Mohammed, Mounir Moussa, Franck Said Abderemane, Rakoarimanana Falinurina na Chadhuili Mradabi.
KIKOSI CHA YANGA SC: Deogratius Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Mwinyi Hajji, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Justin Zullu, Simoni Msuva/Emmanuel Martin, Thabani Kamusoko, Amissi Tambwe/Juma Mahadhi, Obrey Chirwa na Haruna Niyonzima/Said Juma ‘Makapu’.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.