Habari za Punde

YANGA YATINGA HATUA YA PILI, YAWAFUNGASHIA VILAGO NG'AYA YA COMORO,SASA KUKIPIGA NA ZANACO

 Wachezaji wa Yanga wakimpongeza mwenzao Haji Mwinyi, baada ya kuifungia timu yake bao la kusawazisha katika dakika ya 43 kipindi cha kwanza. Bao la Ngaya lilifungwa katika dakika ya 19 pia kipindi cha kwanza, ambapo mchezo huo umemalizika kwa sare ya bao 1-1.
 Haji Mwinyi akimtoka beki wa Ngaya.
************************************************************
Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar
Wawakilishi Tanzania Bara katika ligi ya mabingwa Afrika, Yanga sasa itacheza na wakilishi wa Zambia, timu ya Zanaco FC kabla ya kufuzu hatua ya makundi.
Yanga imefikia hatua hiyo baada ya kulazimisha sare ya bao 1-1 dhidi ya Ngaya Club ya Comoro na kufanikiwa kufuzu hatua hiyo kwa idadi ya mabao ya kufunga 6-2.
Zanaco imefuzu hatua hiyo baada ya kushinda mabo 1-0 dhidi ya APR ya Rwanda mjini, Kigali mapema leo. Yanga itaanzia nyumbani Machi 10 kabla ya kusafiri kwenda Lusaka Machi 17.
Yanga inahitaji kushinda mechi hiyo ili iweze kufuzu katika hatua ya makundi na baaaye robo fainali, kabla ya kucheza nusu fainali na fainali.
Ngaya ilianza mchezo kwa kasi na kutafuta mabao ya kuwawezesha kufuzu katika hatua inayofuata na kupata bao la kuongoza katika dakika ya 19 kupitia kwa Zamir Mohamed.
Shuti kali la Zamir lilimbabatiza beki wa Yanga, Vincent Bossou na kumpita kirahisi kipa wake, Deogratius Munish. Baada ya bao hilo,  Yanga ilikuja juu kwa lengo la kutafuta bao la kusawazisha. kusoma zaidi bofya hapa
Juhudi za Yanga ziliishia kwa wachezaji wake kupiga nje au kupoga ‘kiduchu’ na kipa wa Ngaya Said Mmadi kuokoa kirahisi. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Wachezaji wa Yanga walihisi kuwa kuna ‘uchawi’ kwenye lango la Ngaya na kwenda kufukua na kukuta sarafu (senti tano ya Kitanzania) na kuitupa.
Baada ya kutoa sentitano hiyo iliyowekwa na kipa wa Ngaya, Yanga ilisawazisha katika dakika ya 43 kupitia kwa Haji Mwinyi aliyepiga shuti kali la mita 35.
Yanga ilionekana kujiamini zaidi katika mchezo huo na kutengeneza nafasi nyingi za kufunga, hata hivyo, wachezaji wake, Emmanuel Martin,  Juma Mahadi, Simon Msuva na Obrey Chirwa walipoteza nafasi hizo.
Kocha wa Yanga, Juma Mwambusi aliwapongeza wachezaji wake kwa kufuzu hatua hiyo na sasa kufikiria mechi ya Zanaco.
“Tulichotaka ni kufuzu na tumefanikiwa kufikia hatua hiyo, hivyo wachezaji wanastahili kupongezwa, tumefanya makosa mengi, hata hivyo muda tunao na tunaahidi kuyarekebisha katika mechi zijazo,” alisema Mwambusi.
Nahodha wa Ngaya, Said Hachim aliwapongeza wachezaji wenzake kwa matokeo hayo mazuri kwao. Hachim alisema hawakutegemea kutoka sare na Yanga baada ya kupoteza mchezo wa kwanza.
“Tulikuja hapa kwa lengo moja la kuzuia kufungwa, tulifanya makosa katika mchezo wa kwanza na kufungwa mabao 5-1, leng letu limetimia na sasa tunafuraha kubwa sana, Yanga ni timu kubwa sana,” alisema Hachim.
 Kaseke akimpongeza Haji.
 Kipa wa Ngaya, akiruka kudaka mpira kuokoa hatari langoni kwake.
 Msuva akituliza mpora gambani huku kipa wa Ngaya akijiandaa kuokoa
 Beki wa Ngaya akiokoa huku Kaseke akijaribu kukaba
 Chirwa akijaribu kumroka beki wa Ngaya 
 Emmanuel Martin akiruka kuwania mpira na beki wa Ngaya
 Kipa wa Ngaya akiruka kuokoa hatari
 Obrey Chirwa akimtoka beki wa Ngaya
 Deus Kaseke akiwania mpira na beki wa Ngaya
 Thaban Kamusoko akifanya yake
 Kaseke akiwatoka mabeki wa Ngaya


 Juma Mahadhi akijaribu kupiga shuti katikati ya mabeki wa Ngaya
 Msuva akimtoka beki wa Ngaya
 Mahadhi akimfinya beki wa Ngaya


 KIKOSI CHA YANGA SC:
Vicent Bossou, Deogratias Munishi, Juma Abdul, Mwinyi Haji, Kelvin Yondani, Justine Zulu, Simon Msuva, Thaban Kamusoko, Deus Kaseke, Obrey Chirwa na Emmanuel Martin.

BENCHI LA AKIBA:
Ally Mustafa, Hassan Kessy, Said Juma, Vicent Andrew, Nadir Haroub, Oscar Joshua na Juma Mahadhi.
KIKOSI CHA NGAYA:
Said Hachim, Said Mmadi, Chadhuili Mradabi, Said Anfane, Frank Said, Youssouf Ibrahim, Rakotoarimanana Falinirino, Berthe Alpha, Zamir Mohamed, Mounir Moussa na Said Tohir.

BENCHI LA AKIBA:
Ali Ahamada, Kadafi Said, Chabane Saandi, Abdoul  Hafal, Nadjim Nourdine, Adhepeau Denis na Nourdine Said.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.