Habari za Punde

YANGA YAWASILI JIJINI DAR ES SALAAMLEO, YAPOKELEWA NA MASHABIKI LUKUKI, YAINGIA KAMBINI

Kocha Msaidizi wa Timu ya Yanga Mwambusi, akiongozana na baadhi ya wachezaji wa timu yake wakati walipowasili kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere leomchana wakitokea nchini Comoro walikokwenda kucheza mechi ya Kombe la Klabu Bingwa Afrika na timu ya Ngaya, ambako walishinda kwa jumla ya mabao 5-1. Yanga baada ya kuwasili leo wameingia kambini moja kwa moja kujiwinda na mchezo wa marudiano na timu hiyo pamoja na kambi maalum ya kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Bara kati yake na Watani zao wa Jadi Simba unaotarajia kupigwa Feb 25 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar esSalaam.
Kocha Mkuu wa Yanga Lwandamina akiongoza na baadhi ya wachezaji wakati wakitoka nje ya geti la kutokea wageni uwanjani hapo
Baadhi ya wachezaji wakiwa nje ya uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere baada ya kuwasili leomchana.
Mashabiki wa Yanga wakishangilia,kucheza na kuimba kwa furaha baada ya kuipokea timu yao.
Baadhi ya mashabiki wa Yanga wakiishangilia timu yaobaada ya kuwapokea kwenhye Uwanja wa Julius Nyerere leomchana.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.