Habari za Punde

BAADA YA KUTUPIWA VILAGO YANGA, PLUIJM KUTUA SINGIDA UTD?

Aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, Hans Van De Pluijm, akimkabidhi jezi mchezaji mpya wa kimataifa aliyejiunga na Singida United,  Tafadzwa Kutinyu, aliyesajiliwa hivi karibuni kwa mkataba wa miaka miwili. Pluijm baada ya kutupiwa virago na baadhi ya magazeti kuandika kuondoshwa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi kwa kuchelewa kulipa pango, sasa anatarajia kutua timu hiyo kwa jitihada za Waziri wa Mambo ya ndani, Mwigulu Nchemba, ambaye ni Mbunge wa Iramba Magharibi, Singida.
 Waziri wa mambo ya ndani, Mwigulu Nchemba (wa pili kushoto) akimkabidhi jezi mchezi mpya aliyejiunga na timu ya Singida United, Tafadzwa Kutinyu, aliyetokea timu ya Chicken Inn Fc kwa mkataba wa miaka miwili.
***************************************************
ALIYEKUWA Kocha wa Mabingwa watetezi Dar Young Africans, Hans Van De Pluijm, anatarajiwa kutua kuifundisha timu mpya iliyopanda Daraja mwaka huu, iitakayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara msimu ujao. 
Katika kuanza maandalizi na mikakati ya kuifanya kuwa kati ya zitakazokuwa timu bora msimu ujao, Timu ya Singida United ambayo kwa sasa inaongozwa Mwenyekiti wake wa Usajili, Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba, ambaye anamkubari zaidi kocha huyo bado anafanya jitihada za kuhakikisha kocha huyo anatua kikosini hapo.
Wakati alipokuwa akitangazwa kutua Yanga kocha Lwandamina, Mwigulu alionekana kuingilia kati kwa kumshawishi Kocha huyo Mholanzi aliyekuwa anataka kuondoka baada ya kutoshirikishwa katika maamuzi ya kutua kwa Lwandamina, na hatimaye Nchemba alifanikiwa na kumbakisha kikosini lakini tayari kocha huyo ameripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari leo kutolewa vyombo vyake nje kwa kuchelewa kulipapango la nyumba jambo ambalo ni aibu kubwa kwa Wahusika na timu husika.
Uamuzi wa Pluijm kwenda Singida ni moja ya mikakati ya Mwigulu ambaye ameweka nia ya kufanya usajili wa nguvu utakaowashangaza watu wote na sio kuletewa wachezaji watakaokuwa hawana msaada na timu.
Pluijm alikaririwa akisema kuwa atasaini mkataba na moja ya Klabu ya ligi kuu nchini hivi karibuni lakini sio Simba ambapo hatima yake itajulikana hivi karibuni wapi atakapoelekea mholanzi huyo na tayari ameshaonekana katika picha ya pamoja na kiungo wa kimataifa kutoka nchini Zimbabwe aliyesajiliwa hivi karibuni.
Mapema wiki hii, Singida United ilimsajili kiungo wa kimataifa Tafadzwa Kutinyu kutoka Chicken Inn FC kwa mkataba wa miaka miwili ikiwa ni usajili wa awali.
Kutinyu anayecheza ligi ya Zimbabwe atajiunga na Singida United wakati wa dirisha la usajili litakapofunguliwa mwezi June mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.