Habari za Punde

CHADEMA WAMSHAURI RAIS DKT. MAGUFULI KUELEZA SABABU ZA KUTENGUA NAFASI YA UWAZIRI WA NAPE

Makamu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, kuhusu chama hicho kuwateuwa Lawrence Masha na Ezekia Wenje kugombea Ubunge wa Afrika Mashariki pamoja na mambo mbalimbali yayoendelea nchini. Kulia ni Ofisa Habari wa chama hicho, Tumaini Makene.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
***********************************
Na Dotto Mwaibale, Dar
CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimemtaka Rais Dk. John Magufuli kuueleza umma wa Watanzania sababu za kutengua uteuzi wa aliyekuwa Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye.
Katika hatua nyingine kimesema wabunge wa vyama vya pinzani kwa kushirikiana na wabunge wa Chama cha Mapinduzi wanatarajia kuwasha moto katika Bunge la Bajeti linalotarajia kuanza mapema mwezi ujao kulingana na mambo mbalimbali yautendaji wa Serikali ya awamu ya tano.
Akizungumza Makao Makuu ya chama hicho Kinondoni jijini Dar es Salaam leo siku moja baada ya kutenguliwa kwa uteuzi huo Naibu Katibu Mkuu wa chama cha Chadema Bara, John Mnyika alisema kutokana na taarifa ya Ikulu kutoeleza sababu za kutenguliwa kwa nafasi ya Nape hivyo ipo haja kwa Rais kueleeza wazi sababu ya kumuondoa.
"Rais anapaswa kujitokeza kutoa sababu kwanini katika kipindi hichi ambacho kamati iliyoundwa na Waziri kutoa taarifa iliyoeleza wazo makosa yaliyofanywa na Makonda katika siku chache baada ya Rais kumkingia kifua," alisema.
Hata hivyo alisema kuwa matumizi hayo mabaya ya madaraka kwa sasa yamejipenyeza zaidi hali ambayo kwa sasa hayamuhusu Rais Pekeake bali hata watendaji wa vyombo vya dola ambavyo pia vimejidhihirisha kutokana na matukio yanayoendelea ikiwemo matumizi ya silaha kwenye maeneo ambayo hayakuhitajika.
Alisema ipo haja kwa Rais Magufuli kuwaeleza watanzania kuhusiana na baadhi ya maofisa wa ulinzi na usalama waliovamia kituo cha Luninga cha Clouds wakiwa na silaha na walio mtishia bastola Nape kama amewatuma na kama hakuwatuma pia aeleze hadi sasa ameelekeza wachukuliwe hatua gani, akiwa yeye ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama. 
"Naamini safari hii hatutakuwa wabunge wa Chadema au wa vyama vya upinzani pekee bali naamini safari hii Bunge litakuwa kitu kimoja katika kuchukua hatua wakiwemo wabunge wa CCM," alisema.
Kuhusu wabunge walioteuliwa kushiriki katika uchaguzi wa wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, aliwataja walioteuliwa kutoka katika chama hicho kuwa ni Lawrence Macha na Ezekia Wenje.
Alibainisha kuwa wagombea hao walipatikana kutokana na vikao vya siku mbili vya Kamati Kuu ya Chadema vilivyo fanyika hivi Machi 22 na 23 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.