Habari za Punde

CHAMA CHA SOKA MKOA WA IRINGA, CHAITEKA LIPULI FC

Chama cha mpira mkoa wa Iringa, Waichukua rasmi timu ya Lipuli Fc kwa ajili ya Maandalizi ya Ligi kuu.-Kuyava (Mwenyekiti IRFA)
M wenyekiti huyo ameongea na wanahabari kuhusiana na mwenendo wa timu hiyo. 
Kuwa watasimamia timu hiyo ili kuona inafanya vema ligi kuu Tanzanian bara
Pamoja na hilo pia amesema maandalizi ya usajili yameanza kufanyika. 
Wakati mwenyekiti wa Lipuli FC Abuu changawa Majeck amepokea kwa mikono miwili uamuzi huo na kuwa anaunga mkono uamuzi uliochukuliwa na chama cha mpira wa miguu mkoa wa Iringa. 
Japo alisema wapo baadhi ya watu wamekuwa wakichochea migogoro kwa maslahi yao binafsi jambo ambalo analipinga kwa nguvu zote. 
Huku akisitisha kikao chake cha kesho na wadau na wanachama wa lipuli hadi kupisha kikao cha mkuu wa mkoa wa Iringa hapo kesho.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.