Habari za Punde

DKT. MAGUFULI, RAIS WA BENKI YA DUNIA DKT. JIM YONG KIM, WAZINDUA UJENZI WA MAKUTANO YA BARABARA ZA JUU UBUNGO-UBUNGO INTERCHANGE

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim, kwa pamoja wakifunua kitambaa kuashiria uwekaji wa jiwe la Msingi katika Mradi wa ujenzi wa Makutano ya barabara za Juu Ubungo Interchange jijini Dar es Salaam, leo mchana. Kulia ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akipiga makofi.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Benki ya Dunia Dkt. Jim Yong Kim na baadhi ya viongozi kwa pamoja wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa kuanza kwa ujenzi wa Barabara hizo za juu Ubungo Interchange.
 wakifurahia baada ya kukata utepe huo.
 Rais Dkt. John Magufuli, akihutubia katika hafla hiyo huku akimtaka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,kuendelea kuchapa kazi na kujiepusha na kuyafumbia macho yanayoendelea mitandaoni kuhusu yeye kutochukua hatua kwa yale yanayosemwa juu ya Mkuu huyo wa Mkoa.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akipiga makofi kuashiria kushukuru baada ya kauli hiyo.
 Mwakilishi mkaazi waBenki ya Dunia, Bella Bird (kushoto) akitiliana saini na Waziri wa Fedha, Phillip Mpango, mikataba mitatu ya Maendeleo Mijini, Miradi ya Maji na ujenzi wa Fly Over, leo wakati wa hafla ya uzinduzi na uwekaji Jiwe la msingi ujenzi wa Barabara za juu za Ubungo-Ubungo Interchange.
 Wakibadilishana mikataba baada ya kusainiana
 Mkuu wa MKoa wa Dar es Salaam, akipanda jukwaa kuu kumshukuru Mhe. Rais
 Sehemu ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam,waliojitokeza kushuhudia uzinduzi huo wakimshangilia Raid Dkt. Magufuli wakati akiondoka mahala hapo.
 Wasanii wa Muziki wa Asili kutoka Mkoani Mbeya, Wamwiduka wakitoa burudani wakati wa hafla hiyo
 Rais Dkt. Magufuli na mgeni wake wakishuka katika usafiri wa Mwedno kasi kuingia eneo lililokuwa likifanyika uzinduzi huo. 
 Kundi la Sanaa kutoka mkoani Ruvuma, likitoa burudani ya ngoma ya Mganda katika hafla hiyo.
Wasanii wa kundi la Sanaa la JKT wakishambulia jukwaa katika uzinduzi huo. Picha Zote na MUhidin Sufiani (MAFOTO)

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.